• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za watumishi |
Mbeya District Council
Mbeya District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya Mbeya

  • Nyumbani
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha
      • Ujenzi
      • Mifugo na uvuvi
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango, ufuatiliaji na Takwimu
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA na Mahusiano
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ugavi
      • Elimu msingi
      • Afya
      • Ardhi na Maliasili
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ufugaji wa nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Wataalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Visiting Chairperson
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Mwongozo wa Matumizi ya Vifaa vya TEHAMA
    • Ripoti
      • Mpango Mkakati
      • Council Financial Report
      • Mapato na Matumizi ya Mwezi
      • Council Development Report
      • Annual Performance and Financial Report
      • Mihtasari ya Mikutano ya Baraza
      • Medium Term Expenditure Framework
    • Fomu mbalimbali
      • Leseni za vileo
    • Sheria ndogo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Picha mwendo
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Matukio

Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo

Imewekwa: November 13th, 2017

Kamati ya Fedha, Uongozi  na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imefanya ziara ya siku tatu ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri hiyo. Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni miradi ambayo imepata fedha katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/2018 inayoanzia tarehe 1, Julai 2017 na kuishia tarehe 30 Septamba 2017.

Akiongea wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Mhe. Mwalingo Kisemba amesema kuwa, kwa mujibu wa kanuni zinazoziongoza Halmashauri zinasema kwamba Halmashauri ni lazima iwe na kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, ambayo moja ya majukumu lake ni kukagua miradi ya maendeleo.

“Halmashauri ili iweze kutekeleza majukumu yake ni lazima iwe na kamati mbalimbali ikiwemo kamati ya Fedha ambayo inajumuisha wenyeviti wa kamati nyingine zote. Kamati hii inajukumu kubwa kwanza kupitisha fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Lakini pia inajukumu la kwenda “site” kukagua utekelezaji wa miradi hiyo. kazi hii inafanyika kila robo, yaani kila baada ya miezi mitatu na hii inatekelezwa kwa matakwa ya sheria”

Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Mhe. Julius Ntokani amesema kuwa ziara kama hiyo zinazofanywa na Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango zinafaida kubwa ikiwemo kuchochea kasi ya ukamilishwaji wa miradi ya maendeleo.

Aidha Mhe. Ntokani amesema kuwa faida nyingine zinazopatikana kwenye ziara hizo ni kukutana na wananchi ambapo wanapata nafasi ya kuwahasisha kuchangia juu ya ujenzi wa miradi hiyo kwa kushirikiana na Halmashauri.

“Ziara hizi zinazofanywa na Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, zimekuwa na faida nyingi ikiwemo kuchochea kasi ya ukamilishaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa sababu kwenye ziara hizo tunaongozana na wataalamu wa Halmashauri, hivyo kwenye kila mradi tunapokea taarifa ya utekelezaji. Baada ya kupokea taarifa hizo tunaanza kukagu mradi. Tukisha kagua tunawaambia wataalamu mapungufu tuliyoyabaini kisha wataalamu wanayafanyia kazi hali inayopelekea miradi hiyo kukamilika kwa wakati na kwa ubora uliokusudiwa”

Lakini pia kwenye ziara hizi sisi kama madiwani tunapata fursa ya kukutana na wananchi, tunapokutana nao tunawaeleza faida za wao kuchangia katika miradi ya maendeleo hali inayoipelekea kuipunguzia gharama Hamashauri”

Katika ziara hiyo kamati ya fedha imeweza kukagua jumla ya miradi nane ambayo ni; machinjio ya kisasa ya Utengule, Hosteli ya wasichana Shule ya Sekondari Iwindi, kivutio cha Utalii cha chemichemi ya maji moto Ilota, daraja la Idiwili, Kituo cha Afya Isuto, jengo la Utawala Shule ya Sekondari Iyelanyala, jengo la Utawala Shule ya Sekondari tarajiwa ya Wasichana Galijembe, na shule ya Sekondari Ntonzo.

Katika iradi hiyo, miradi sita inatekelezwa na Halmashauri kwa kushirikiana huku miradi miwili ya Kivutio cha Utalii chemichemi ya maji moto Ilota na Shule ya Sekondari Ntonzo inatekelezwa na watu binafsi.

Kaimu Afisa Mipango Wilaya, Ndg. Firbert Mbwilo amesema kuwa kamati hiyo pia imepita kwenye miradi inayotekelezwa na watu binafsi kwa lengo la kujifunza. Mbwilo amesema Halmashauri inakumbana na changamoto mbalimbali wakati wa kutekeleza miradi yake, na inapaswa kutafuta mbinu za kukabilana na changamoto hizo.  Hivyo Halmashauri inalazimika kutembelea sekta binafsi haswa zile zinazofanya vizuri kujifunza zaidi katika kuboresha hudama zake.

 

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa Kazini Watendaji wa Vijiji 85 na Madereva Wawili October 16, 2017
  • TANGAZO LA KUWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UGONJWA WA KIPINDUPINDU November 13, 2017
  • Tazama zote

Habari mpya

  • Mradi wa Maji Izumbwe, Iwindi, Mwashiwawala kukamilika mwezi Juni, 2018

    April 02, 2018
  • Serikali iondoe chuki ya wananchi kwa kusimamia vyema miradi ya maendeleo- Mhe. Mwakasole, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya

    March 27, 2018
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imetekeleza ahadi yake ya kutoa mikopo kwa wanawake na vijana kila baada ya miezi mitatu

    March 22, 2018
  • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo

    November 13, 2017
  • Tazama zote

Video

Vifaa Tiba
Picha mwendo zaidi

Linki za haraka

  • Mbeya Region Website

Tovuti zinazohusiana

  • Public Service Management website
  • e Goverment Agency
  • PORALG

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Mbaliz Road

    Sanduku la posta: 599

    Simu ya mezani: 025-2502260

    Simu ya mkononi: 0762210758

    Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera binafsi
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma zetu

Hakimiliki@2018GWF. Haki zote zimehifadhiwa