• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za watumishi |
Mbeya District Council
Mbeya District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya Mbeya

  • Nyumbani
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mifugo na uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA na Mahusiano
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi
      • Ufugaji wa nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Wataalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
      • Taarifa ya fedha
      • Mpango wa Mapato na Matumizi
      • Mapato na Matumizi ya Mwezi
      • Taarifa ya miradi ya maendeleo
      • Taarifa ya fedha ya mwaka
      • Mihtasari ya Mikutano ya Baraza
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
      • Mwongozo wa Matumizi ya Vifaa vya TEHAMA
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Picha mwendo
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

DC ITUNDA AHIMIZA KUSIMAMIA MAPATO KWA MAENDELEO

Imewekwa: February 3rd, 2026


Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Solomon Itunda, amewataka Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kusimamia kwa umakini ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo.

Mheshimiwa Itunda ametoa wito huo wakati akihutubia kikao cha pili cha ufunguzi wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya (Mbeya DC), kilichofanyika leo, tarehe 03 Februari 2026.


Amesema kuwa Madiwani wanapaswa kushirikiana kwa karibu na Watendaji wa Serikali katika ngazi ya kata na vijiji ili kuimarisha juhudi za ukusanyaji wa mapato ya ndani, kwa lengo la kufikia asilimia 100 ya makusanyo ifikapo mwezi Juni 2026.

Aidha, DC Itunda amesisitiza umuhimu wa Madiwani kusimamia kwa karibu matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo zinazotolewa na Serikali Kuu, hususani miradi mikubwa ya kimkakati, ili kuhakikisha thamani ya fedha inazingatiwa katika kila mradi unaotekelezwa kwenye kata zao.


Akizungumzia miradi hiyo ya kimkakati, DC Itunda amesema Serikali tayari imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Kata ya Igawa hadi Tunduma yenye thamani ya shilingi bilioni 183. Awali, mradi huo ulikuwa na thamani ya shilingi bilioni 128, lakini Serikali iliongeza shilingi bilioni 55 ili kuimarisha utekelezaji wake.

Vilevile, Serikali imetoa shilingi bilioni 119 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji kutoka Kata ya Kiwira, iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, ambao unalenga kumaliza changamoto ya maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya na Halmashauri ya Jiji la Mbeya. Kwa sasa, mradi huo umefikia asilimia 50 ya utekelezaji wake.


DC Itunda ameongeza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imefanikiwa kutekeleza zoezi la kupeleka umeme vijijini kwa asilimia 95, hatua itakayosaidia wananchi kupata nishati safi na bora kwa ajili ya maendeleo ya shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Kwa upande mwingine, amebainisha kuwa Serikali imetoa shilingi bilioni 2.7 kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya la Halmashauri, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.

Matangazo

  • VITUO VYA KUJIANDIKISHIA ORODHA YA WAPIGA KURA October 11, 2024
  • TANGAZO LA KAZI YA KUJITOLEA KWA KAZI YA MSAIDIZI WA WATOTO MAHAKAMANI February 02, 2022
  • TANGAZO LA ZOEZI LA UTOAJI WA ANWANIZA MAKAZI March 04, 2022
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA March 16, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • DC ITUNDA AHIMIZA KUSIMAMIA MAPATO KWA MAENDELEO

    February 03, 2026
  • MBEYA DC YAPOKEA VIFAA KUWEZESHA MASIJALA MTANDAONI

    February 03, 2026
  • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Yakamilisha Ziara ya Ukaguzi.

    January 21, 2026
  • MIRADI YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 800 YAKAGULIWA NA FUM

    January 20, 2026
  • Tazama zote

Picha Mwendo

"Wapo Wakuu wa Idara na Vitengo wakiamishwa watu wanafanya sherere" Waitara Naibu waziri TAMISEMI
Picha mwendo zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MBEYA

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti ya mkoa wa Mbeya

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

writingMasterThesis

Mahali

Wasiliana nasi

    Mbaliz Road

    Sanduku la posta: 599

    Simu ya mezani: 025-2502260

    Simu ya mkononi: 0762210758

    Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera binafsi
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma zetu

Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.