Timu ya Mpira wa Miguu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya (Mbeya DC) imelazimishwa sare ya magoli 4–4 dhidi ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Watumishi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST) katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha MUST, Jijini Mbeya.
Katika mchezo huo uliokuwa wa kasi na ushindani mkubwa, Timu ya Watumishi wa MUST ilianza vyema kwa kufunga magoli mawili ya mapema. Hata hivyo, Mbeya DC ilijibu kwa haraka na kusawazisha magoli hayo.
Mchezo uliendelea kwa mtindo wa piga nikupige hadi filimbi ya mwisho ilipopulizwa, ambapo timu zote zilionyesha uwezo na ushindani mkubwa na hatimaye kutoshana nguvu kwa sare ya magoli 4–4.
Magoli ya Mbeya DC yalifungwa na nyota wao wanne, ambao ni Richard Mwakalinga, Oscar Baganda, Imani Kagesya, na Said Mlau.
Aidha, katika mchezo mwingine wa mpira wa wavu (volleyball) uliochezwa sambamba na mechi ya mpira wa miguu leo katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha MUST, Timu ya Mpira wa Wavu ya Mbeya DC ilishindwa kufua dafu mbele ya Timu ya Mpira wa Wavu ya MUST, na kuruhusu kupoteza kwa seti 4–2.

Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.