• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za watumishi |
Mbeya District Council
Mbeya District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya Mbeya

  • Nyumbani
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mifugo na uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA na Mahusiano
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi
      • Ufugaji wa nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Wataalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
      • Taarifa ya fedha
      • Mpango wa Mapato na Matumizi
      • Mapato na Matumizi ya Mwezi
      • Taarifa ya miradi ya maendeleo
      • Taarifa ya fedha ya mwaka
      • Mihtasari ya Mikutano ya Baraza
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
      • Mwongozo wa Matumizi ya Vifaa vya TEHAMA
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Picha mwendo
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

MKURUGENZI, WATENDAJI VIJIJI MBEYA DC WAJADILI MIKAKATI KUHARAKISHA MAENDELEO

Imewekwa: February 12th, 2026

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya (Mbeya DC), Bi. Erica Yegella, leo amefanya kikao kazi maalum na Watendaji wa Vijiji (VEOs) kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji, ikiwemo fursa zilizopo, changamoto zinazowakabili, pamoja na mikakati ya kukabiliana nazo ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi.

Katika kikao hicho, Bi. Yegella aliwasisitiza Watendaji wa Vijiji kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma. Aliwataka kuwa na unyenyekevu na kuwaheshimu Wenyeviti wa Vijiji, ambao ni wawakilishi halali wa wananchi katika maeneo yao.

“Niwaombe tuwaheshimu sana Wenyeviti wa Vijiji. Tufanye kazi kwa unyenyekevu na upendo, kwa sababu unyenyekevu ni sifa muhimu ya kiongozi. Kumbukeni kuwa ninyi ni wasimamizi wakuu katika vijiji vyenu; vitongoji vyote vinawategemea na kuwasikiliza. Msipokuwa wanyenyekevu, wenye utii na kuheshimu viongozi wenzenu, itakuwa vigumu kutekeleza majukumu yenu ipasavyo,” alieleza Mkurugenzi Mtendaji huyo.

Bi. Yegella alisisitiza zaidi kuwa Watendaji wa Vijiji ni kiungo muhimu kati ya Halmashauri na wananchi katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Hivyo, aliwataka kujiepusha na mambo yasiyo ya msingi na badala yake kutimiza wajibu wao kwa weledi na uwajibikaji.

Alielekeza kwamba pale wanapokumbana na changamoto au kutoelewa jambo, wawasiliane kwanza na Watendaji wa Kata; na endapo nao watashindwa kutoa ufafanuzi, basi wawasiliane na Watumishi wa Idara ya Utawala na Utumishi ngazi ya Halmashauri.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo aliwahimiza Watendaji wa Vijiji kutumia ipasavyo mifumo ya kidijitali katika malipo na usimamizi wa fedha, ili kurahisisha uandaaji wa hesabu, hususani mwishoni mwa mwaka wa fedha. Alisisitiza kuwa kila Mtendaji wa Kijiji anapaswa kuielewa vizuri mifumo ya malipo, kwa kuwa wao ndio wasimamizi wakuu wa shughuli za kiutawala na kifedha katika vijiji.

“Sasa hivi hatufanyi malipo kwa mkono kwa kutumia makaratasi. Kila kitu kinafanyika kupitia mifumo ya kidijitali. Hata mishahara hailipwi tena kwa kupanga foleni kama ilivyokuwa zamani wakati wa matumizi ya stakabadhi za kuandika kwa mkono (HW5),” alifafanua Mkurugenzi huyo.

Akihitimisha kikao hicho, aliwataka Watendaji wa Vijiji kuhakikisha hawatoi fedha benki bila kuwa na nakala ya muamala kutoka katika mfumo wa FFAIRS pamoja na muhtasari wa kikao husika. Alisisitiza kuwa hatua hiyo ni ya lazima, na kwamba mihtasari ya vikao vyote vya kamati lazima iambatane na nakala kutoka kwenye mfumo ili kuruhusu utoaji wa fedha.

Matangazo

  • VITUO VYA KUJIANDIKISHIA ORODHA YA WAPIGA KURA October 11, 2024
  • TANGAZO LA KAZI YA KUJITOLEA KWA KAZI YA MSAIDIZI WA WATOTO MAHAKAMANI February 02, 2022
  • TANGAZO LA ZOEZI LA UTOAJI WA ANWANIZA MAKAZI March 04, 2022
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA March 16, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MBEYA DC YASAJILI 483 BIMA YA AFYA KWA WOTE

    February 13, 2026
  • MWENYEKITI MBEYA DC AKABIDHI VISHIKWAMBI 44 KWA MADIWANI KUIMARISHA UFANISI WA KAZI

    February 13, 2026
  • MKURUGENZI, WATENDAJI VIJIJI MBEYA DC WAJADILI MIKAKATI KUHARAKISHA MAENDELEO

    February 12, 2026
  • MBEYA DC YASISITIZA MATUMIZI SAHIHI MIKOPO YA ASILIMIA 10

    February 11, 2026
  • Tazama zote

Picha Mwendo

"Wapo Wakuu wa Idara na Vitengo wakiamishwa watu wanafanya sherere" Waitara Naibu waziri TAMISEMI
Picha mwendo zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MBEYA

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti ya mkoa wa Mbeya

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

writingMasterThesis

Mahali

Wasiliana nasi

    Mbaliz Road

    Sanduku la posta: 599

    Simu ya mezani: 025-2502260

    Simu ya mkononi: 0762210758

    Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera binafsi
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma zetu

Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.