Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya Erica Yegella, ametembelea banda la Halmashauri hiyo kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Halmashauri yake katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, maonyesho yanayoendelea ndani ya uwanja wa John Mwakangale (Nanenane) Uyole Mbeya mjini.
Baada ya kutembelea banda hilo, mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya amewapongeza maafisa mbalimbali katika banda hilo hususani sekta ya kilimo na uvuvi na kuwaasa kuendelea kutangaza fursa mbalimbali zilizopo wilayani Mbeya hususani jimbo la Mbeya vijijini (Halmashauri ya wilaya ya Mbeya).
Bi. Yegella, ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wananchi wote wakiwemo wakulima kutembea banda la Halmashauri ya Mbeya ndani ya viwanja vya Nanenane Mbeya ili kujifunza fursa mbalimbali kwenye eneo la Mifugo, Kilimo na Uvuvi kwani kwa asilimia kubwa Halmashauri hiyo inafanya vizuri kwenye upatikanaji na ukusanyaji wa mapato kutokana na kufanya vizuri kwenye eneo la Kilimo na biashara hivyo kueleza Halmashauri hiyo (Mbeya DC) kuwa mfano katika kueneza kilimo bora kwa wananchi ambako kumekuwa kukishuhudiwa mashamba darasa kwa ajili ya kuendelea kuwafundisha wananchi Kilimo bora na kuhama kutoka kwenye kilimo cha mazoea kwenda kwenye kilimo bora na kubadilisha maisha yao.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.