Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya Erica E. Yegella, ametembelea shule ya sekondari Usongwe iliyopo katika kata ya Utengule Usongwe mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi wilayani Mbeya na kukagua ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike katika shule hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya uongozi wa shule hiyo ya upili, bweni hilo katika shule ya Sekondari Usongwe ni muhimu na litakuwa na uwezo wa kubeba wanafunzi mia tatu kwa wakati mmoja.
Akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali katika sekta ya elimu akiwemo afisa elimu sekondari Mwal. Aliko Mbuba, mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbeya Erica Yegella amesisitiza uaminifu na kuzingatia muda wa utekelezaji wa mradi huo ili kukamilika kwa wakati na baadaye kuanza kutumika na wanafunzi ili kusaidia kuboresha zaidi ufaulu shuleni hapo.
DED Yegella amesema Serikali ya awamu ya sita inatumia mamilion ya fedha kuimarisha miundombinu mbalimbali kwa wananchi wake ikiwemo kwenye kada ya elimu ili kusaidia watoto kuishi, kusoma na kujifunzia kwenye mazingira safi na salama kwani elimu ndio msingi thabiti wa maisha yao na Tanzania ijayo.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.