BARAZA LA MADIWANI
Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya inaongozwa na Baraza la Madiwani ambalo ndio chombo cha juu cha maamuzi yote ya Halmashauri. Baraza la madiwani la Halmshauri ya Wilaya ya Mbeya linaundwa na jumla ya Waheshimiwa Madiwani 39 huku likiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kusaidiana na Makamu wake.
Baraza la Madiwani linapitisha maamuzi yake kupitia mikutano ya Halmashauri. Kuna aina nne za Mikutano ya Halmashauri kama ilivyotafsiriwa kwenye Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya za Mwaka 2013. Mikutano hiyo ni; Mikutano ya kawaida ya Halmashauri, Mkutano Maalumu, Mkutano wa Bajeti na Mkutano wa Mwaka.
Mikutano ya Kawaida ya Halmashauri, hii ni mikutano inayofanyika mara nne kwa mwaka; yaani mkutano mmoja kila baada ya miezi mitatu.
Mkutano Maalum wa Halmashauri, huu ni Mkutano unaoitishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ama Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ndani ya siku ishirini na moja (21) baada ya kupokea kwa maandishi maombi ya kuitishwa Mkutano huo toka kwa waheshimiwa madiwani. Kama Mkutano utaitishwa na Mwenyekiti barua ya maombi inapaswa kusainiwa na idadi isiyopungua theluthi moja ya madiwani wote huku ikielezea wazi madhumuni ya kuomba kuitishwa mkutano huo.
Lakini kama madhumuni ya kuomba kuitishwa Mkutano huo ni kumuondoa Mwenyekiti madarakani barua ya maombi inapaswa kusainiwa na theluthi mbili ya idadi ya Waheshimiwa madiwani wote na kuwasilishwa kwa Mkurugenzi Mtendaji ambaye ataitisha Mkutano huo ndani ya siku ishirini na moja (21)
Mkutano huu hauna idadi kamili ya kufanyika kwa mwaka, bali unaweza kuitishwa wakati wowote linapoibuka jamba la dharula.
Mkutano wa Bajeti, huu ni Mkutano unaofanyika mara moja kwa mwaka kwa siku mbili mfululizo. Lengo kuu la Mkutano huu ni kupitia taarifa ya Utekelezaji wa mpango wa bajeti ya mwaka uliopita na kupitisha mpango wa bajeti wa mwaka unaofuata.
Mkutano wa Mwaka wa Halmashauri, Mkutano huu unaitishwa na Mkurugenzi Mtendaji kwa kuwasiliana na Mwenyekiti wa Halmashauri. Mkutano huu unaitishwa mara moja kwa mwaka ambapo mambo manne yanafanyika katika Mkutano huu, mambo hayo ni; kufanya uchaguzi wa kumchagua Makamu wa Mwenyekiti, kuteua na kupitisha Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Halmashauri; kujadili taarifa ya utendaji na uwajibikaji wa Halmashauri kwa mwaka uliopita na kupitisha ratiba ya vikao vya Halmashauri na Kamati za Halmashauri.
KAZI ZA BARAZA LA MADIWANI
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.