• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za watumishi |
Mbeya District Council
Mbeya District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya Mbeya

  • Nyumbani
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mifugo na uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA na Mahusiano
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi
      • Ufugaji wa nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Wataalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
      • Taarifa ya fedha
      • Mpango wa Mapato na Matumizi
      • Mapato na Matumizi ya Mwezi
      • Taarifa ya miradi ya maendeleo
      • Taarifa ya fedha ya mwaka
      • Mihtasari ya Mikutano ya Baraza
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
      • Mwongozo wa Matumizi ya Vifaa vya TEHAMA
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Picha mwendo
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Maendeleo ya Jamii

IDARA YA MAENDELEO YA JAMII

UTANGULIZI:

Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ina jumla ya watumishi 41 wanawake 22 wanaume 19. Idara inatekeleza majukumu yak echini ya  vitengo 7 ambavyo ni  Kitengo cha Vijana, Dawati la uwezeshaji kiuchumi, Dawati la  jinsia , Uratibu wa program ya UKIMWI, TASAF, Uratibu wa asasi, Dawati la watoto na Dawati la vizazi na vifo(RITA)

MAJUKUMU YA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII KULINGANA NA VITENGO

SEHEMU A; PROGRAM YA UKIMWI

UTANGULIZI

Tangu kugundulika kwa UKIMWI mwanzomi mwa miaka ya 1980, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imekuwa ikitekeleza shughuli mbalimbali zinazolenga kupunguza kasi ya maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI pamoja na kuboresha huduma za UKIMWI kwa watu wanaoishi na maambukizi hayo. Haya yote yamekuwa yakitekelezwa na Halmashauri kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali zikiwemo Asasi zisizo za kiserikali, Mashirika na taasisi mbalimbali pamoja na Kamati mahsusi kwa ajili ya usimamizi na utekelezaji wa shughuli za UKIMWI zilizoundwa kuanzia ngazi ya kijiji hadi wilaya.

Hadi sasa, kasi ya maambukizi mapya ya Virusi Vya UKIMWI ni ile inayoakisiwa na kiwango cha maambukizi cha kimkoa ambacho ni 9.0%. Hata hivyo kiwango hiki kimeshuka kutoka 9.2 Kwa mwaka 2010 na utafiti mwingine unafanyika mwaka huu wa 2017.

SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA NA PROGRAM YA UKIMWI

  • Kuratibu, kupanga na kusimamia utekelezaji wa shughuli zote za VVU
  • na UKIMWI zinazotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
  • Kuandaa na kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa
  • shughuli za program ya UKIMWI za kila robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mzima na kuziwasilisha ngazi ya Halmashauri na Mkoa.
  • Kubaini mahitaji na kuandaa mpango kazi wa kujenga uwezo
  • miongoni mwa wadau wanaoshughulika na afua za UKIMWI katika
  • Halmashauri.
  • Kufuatilia, kutathimini na kubaini  vichocheo vya maambukizo ya VVU na maeneo hatarishi yanayosababisha kasi kubwa ya maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI.
  • Kuwa kiungo kati ya Halmashauri na wadau wengine katika utekelezaji wa shughuli za VVU na UKIMWI katika Halmashauri.

 

MAFANIKIO YALIYOFIKIWA.

  • Uwepo wa Kamati shirikishi za kudhibiti UKIMWI kuanzia ngazi ya Vijiji, Kata na Wilaya zilizoundwa kwa kuzingatia mwongozo wa mwaka 2014.
  • Uwepo wa mabaraza ya watu waishio na maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI kwa ngazi za Kata na Wilaya ambayo yamekuwa msaada mkubwa katika kutetea na kusimamia haki na wajibu wa watu waishio na maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI.
  • Mwitikio mkuwa wa watu waishio na maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI kujiunga katika vikundi ili kutengeneza umoja kati yao na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwao. Hadi sasa kuna jumla ya vikundi 73 vya watu waishio na maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI ambavyo kati ya hivyo, vikundi 57 vimesaidiwa na Halmashauri kwa kuanzishiwa miradi ya ufugaji wa mbuzi wa maziwa na kuku.
  • Kuboreshwa kwa utoaji wa huduma za UKIMWI kwa watu waishio na maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI ambapo hadi sasa jumla ya vituo (CTC) 9 vinatoa huduma ya tiba na matunzo kwa watu waishio na maambukizi. Aisha vituo 6 vimeanzishiwa huduma mkoba (mobile CTC) ili kuwafikia watu wengi zaidi.

CHANGAMOTO

Pamoja na mafanikio hayo yaliyofikiwa, bado kuna changamoto ambazo zimekuwa zikikwamisha ufikiaji wa malengo kwa wakati. Miongoni mwa changamoto hizo ni;

  • Uchache wa rasilimali hasa rasilimali fedha katika kuwafikia walengwa wengi zaidi na kwa wakati.
  • Uchache wa mashirika (asasi) yanazotekeleza shughuli za UKIMWI ambapo mashirika mengi yapo Halmashauri zilizoko mijini zaidi kuliko zile zilizoko pembezoni. Hii inasababisha kutokuwa na nguvu ya pamoja inayotosheleza katika kupambana na UKIMWI.

HITIMISHO

Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kupitia Program ya UKIMWI itaendelea kutafuta rasilimali fedha kutoka vyanzo vingine vya mapato ili kuongeza nguvu ya mapambano. Aidha, itaendelea kushirikiana na wadau waliopo na wengine watakaoendelea kuja katika kuunga mkono mwitikio wa kitaifa wa kupambana na UKIMWI ili kufikia “Sifuri 3” ifikapo mwaka 2030, yaani kutokomeza kabisa maambukizi mapya ya Virusi Vya UKIMWI, Unyanyapaa na Vifo vitokanavyo na UKIMWI.

SEHEMU B; DAWATI LA WATOTO

UTANGULIZI

Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya pamoja na kazi nyingine zinazotekelezwa, pia inasimamia haki na ulinzi wa mtoto kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Mtoto namba 21 ya mwaka 2009 kuwa mtoto ni mtu yeyote mwenye umri chini ya miaka kumi na nane (18). Kutokana na sensa ya mwaka 2012, hadi sasa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ina jumla ya watoto 164,339 kati yao watot wa kike ni 83,453 na watoto wa kiume ni 80,886.

 

 

SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA NA DAWATI LA WATOTO

  • Kuratibu, kupanga na kusimamia utekelezaji wa shughuli zote za watoto zinazotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
  • Kuandaa na kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa
  • shughuli za dawati la watoto za kila robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mzima na kuziwasilisha ngazi ya Halmashauri na Mkoa.
  • Kubaini mahitaji na kuandaa mpango kazi wa kujenga uwezo
  •     miongoni mwa wadau wanaoshughulika na afua za watoto katika
  • Halmashauri.
  • Kufuatilia, kutathimini na kubaini  vichocheo vya matukio ya    ukatili na unyanyasaji kwa watoto. Kuwa kiungo kati ya Halmashauri na wadau wengine katika utekelezaji wa shughuli za watoto katika Halmashauri.
  • Kutoa elimu kwa jamii juu ya malezi na makuzi ya watoto
  • Kutafsiri na kuelimisha Sera, Sheria na miongozo mbalimbali inayohusu maendeleo ya mtoto.
  • Kufanya ufuatiliaji wa Kamati zinazoshughulikia masuala ya ulinzi na usalama wa mtoto.
  • Kuratibu na kusimamia mabaraza ya watoto, Klabu za watoto kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali
  • Kutafuta na kutunza takwimu zinazohusu watoto na kutambua watoto wenye mahitaji maalum.

MAFANIKIO YALIYOFIKIWA.

  • Uwepo wa Kamati na mabaraza ya watoto katika kata zote 28
  • Mwitikio mkubwa wa jamii na wadau mbalimbali katika kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum hasa kielimu na afya.
  • Kuongezeka kwa uelewa wa masuala ya watoto ambako kumewapa watoto na jamii nzima uwezo wa kujiamini na kutoa taarifa mbalimbali za matukio ya ukatili na unyanyasaji kwa watoto.
  •  

CHANGAMOTO:

Pamoja na mafanikio hayo yaliyofikiwa, bado kuna changamoto ambazo zimekuwa zikikwamisha ufikiaji wa malengo kwa wakati. Miongoni mwa changamoto hizo ni;

  • Uchache wa rasilimali hasa rasilimali fedha katika kuwafikia walengwa wengi zaidi na kwa wakati.
  • Uchache wa mashirika (asasi) yanazotekeleza shughuli za watoto ambapo mashirika mengi yapo Halmashauri zilizoko mijini zaidi kuliko zile zilizoko pembezoni. Hii inasababisha kutokuwa na nguvu ya pamoja inayotosheleza katika kupambana na watoto.
  • Ukubwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya na namna ilivyokaa inasababisha ugumu wa kuyafikia maeneo yote kwa wakati.

 

HITIMISHO

Pamoja na mafanikio yaliyofikiwa, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kupitia Dawati la Watoto itaendelea kutekeleza shughuli zote zenye lengo la kutokomeza kabisa vitendo vya ukatilli na unyanyasaji kwa watoto pamoja na kusimamia Sera na Sheria ya Mtoto kwa ustawi wa watoto.

  • SEHEMU C: URATIBU WA VIZAZI NA VIFO

UTANGULIZI

Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ni miongoni mwa Halmashauri zinazofanya uratibu wa vizazi na vifo kwa watoto chini ya miaka mitano (5) na zaida ya miaka mitano. Halmashauri hii ina jumla ya kata 28 na vituo vya tiba 87 vinavyofanya usajili wa vizazi (vyeti vya kuzaliwa) kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano na watoto zaidi ya miaka mitano vinatolewa kwenye Makao Makuu ya Ofisi za Halmashauri. Mpango huu ulianza Julai 2013 ambao unaratibiwa na Idara ya Maendeleo ya Jamii.

 

SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA

  • Kuratibu, kupanga na kusimamia utekelezaji wa shughuli zote za usajili wa vizazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
  • Kuandaa na kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa
  • shughuli za vizazi za kila robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mzima na kuziwasilisha ngazi ya Halmashauri na Mkoa.
  • Kuandaa mpango kazi na kuwajengea uwezo wasajiri na wananchi kwa ujumla.
  • Kufanya ufuatiliaji wa shughuli za usajiri wa vizazi kwenye vituo vya tiba na kwenye kata.
  • Kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa vyeti vya kuzaliwa.
  • Kutafsiri na kuelimisha jamii juu ya Sera, Sheria na Miongozo mbalimbali inayohusu uandikishaji wa yeti vya kuzaliwa.
  • Kutafuta na kutunza takwimu zinazohusu usajili wa vizazi.

MAFANIKIO YALIYOFIKIWA.

  • Mwitikio mkubwa wa jamii katika kuchukua vyeti vya kuzaliwa.
  • Kuongezeka kwa uelewa wa wananchi juu ya umuhimu wa kuwa na vyeti vya kuzaliwa.
  • Kusogeza huduma jirani na wananchi.

CHANGAMOTO:

Pamoja na mafanikio hayo yaliyofikiwa, bado kuna changamoto ambazo zimekuwa zikikwamisha ufikiaji wa malengo kwa wakati. Miongoni mwa changamoto hizo ni;

  • Uchache wa rasilimali hasa rasilimali fedha katika kuwafikia walengwa wengi zaidi na kwa wakati.

 

 

HITIMISHO

Pamoja na mafanikio yaliyofikiwa, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kupitia vituo vya tiba ofisi za kata zitaendelea kutoa na kufanya uhamasishaji nakutekeleza shughuli za utoaji wa vyeti vya kuzaliwa.

SEHEMU D; DAWATI LA UWEZESHAJI WANACHI    KIUCHUMI

UTANGULIZI:

Kitengo cha Dawati la uwezeshaji wananchi kiuchumi ni mojawapo ya vitengo vya Idara ya Maendeleo ya Jamii chini ya baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) ambacho kinafanya shughuli zake kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo ya serikali chini ya sera ya uwezeshaji wa wananchi kiuchumi ya mwaka 2004, katika kuhakikisha mazingira wezeshi kwa wadau kufikisha huduma kwa jamii na maendeleo wao.

SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA

  • Kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa Sera na Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi kiuchumina Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi katika Halmashauri
  • Kukusanya taarifa na tafiti mbalimbalina kumshauri Mkurugenzi Mtendajiwa Halmashauri ya Wilaya katika masuala ya Uwezeshaji Kiuchumi na Ushiriki wa Watanzania
  • Kuhakikisha kuwa Halmashauri inahusisha suala la hifadhi ya mazingira namabadiliko ya Tabia Nchi katika mipango ya maendeleo ya Wilaya ilikuboresha mazingira ambayo nimuhimu katika suala zima la uzalishaji wamazao ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
  • Kubuni na kutafuta vyanzo vya rasilimali kwa ajili ya shughuli za uwezeshaji katika Halmashauri
  • Kuratibu na kuhamasisha uanzishwaji na uendelezaji wa Vikundi vya kiuchumi kama SACCOS, VICOBA na vinginevyo vinavyosajili wanakutambuli wakutoka ngazi yaWilaya hadi Taifa na kujirasimisha na kufanya uzalishaji wenye viwango kama vya TBS na TFDA na kupata nembo ya utambuzi wa bidhaa (msimbomilia (barcode)
  • Kubuni fursa mbalimbali za uwekezaji katika Halmashauri
  • Kushauri namna ya uboreshaji wa vituo vidogo vidogo vya kibiashara hususani katika Vijiji na Kata

MAFANIKIO: 

  • Upatikanaji wa huduma bora za kiuchumi na kijamii na kuboreshwa kwa mazingira wezeshi ya uwekezaji katika jamii na wadau.
  • Ongezeko la vikundi vya kijamii hivyo kupelekea jamii kuondokana umaskini na utegemezi uliokithiri.
  • Ongezeko la vikundi kujisajili na kujirasimisha na kufanya uzalishaji wenye viwango.
  • CHANGAMOTO
  • Uibukaji wa vikundi vingi vilivyoundwa kwa ajili ya dhana ya million hamsini kila kijiji.
  • Kuibuka kwa taasisi binafsi zinazowatapeli wananchi kuunda vikundi kwa dhana ya kupata milioni hamsini kila kijiji.
  • Ugumu wa upatikanaji wa takwimu mbalimbali kutokana na geografia ngumu ya Halmashauri yetu,

SEHEMU E: URATIBU WA ASASI

UTANGULIZI:

Kitengo cha Uratibu wa asasi ni miongoni mwa vitengo vilivyo chini ya Idara ya Maendeleo ya Jamii ambacho kinafanya shughuli zake kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo ya serikali chini ya sheria ya mashirika yasioya kiserikali ya mwaka 2002 katika kuhakikisha mazingira wezeshi kwa wadau kufikisha huduma kwa jamii na maendeleo yao.

MAJUKUMU YA KITENGO CHA URATIBU WA ASASI

  • Kuratibu utendaji kazi wa Asasi zote zinazofanya kazi katika Halmashuri ya Wilaya ya Mbeya
  • Kutoa elimu ya mchakato unaotumika katika usajili wa Asasi
  • Kutoa elimu juu ya Sera, Miongozo na Sheria mbalimbali zinazohusu Asasi
  • Kukusanya takwimu za makundi mbalimbali zinazohusu vikundi vya vijana, WAVIU, Wanawake, Asasi, Watoto wanaoishi katika manzingira hatarishi, walemavu, VICOBA na SACCOS ili kuwa na takwimu zinazoendana na wakati
  • Kusimamia na kufuatilia shughuli za maendeleo ya jamii zinazofanywa na wadau katika kata na vijiji katika Halmashauri
  • Kuratibu na Kuandaa mafunzo mbalimbali kwa jamii/vikundi na  kuviwezesha kukua kiuchumi kwa kuwapa mikopo ya riba nafuu na kusimamia urejeshaji wa mikopo kwa wakati kwa kushirikia na dawati

 

MAFANIKIO

  • Upatikanaji wa huduma bora za kiuchumi na kijamii na kuboreshwa kwa mazingira wezeshi ya uwekezaji katika jamii na wadau.
  • Ongezeko la vikundi vya kijamii vilivyosajiliwa na kujirasimisha hivyo kupelekea jamii kuondokana umaskini na utegemezi uliokithiri.
  •  Uwepo wadau/asasi waliotambuliwa na Halmashauri wanaofanya kazi za kiuchumi na kijamii nafsi katika masuala ya UKIMWI, Ustawi jamii na watoto

CHANGAMOTO:

  • Baadhi ya asasi kutoleta taarifa zao za kazi hasa ambazo hazina ufadhili wautekelezaji shughuli zao kwa wakati.
  • Mwitikio mdogo kwa baadhi ya vikundi katika kusajili

HITIMISHO

  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kupitia kitengo uratibu wa ASASI inawashukuru wadau wanaotumia rasimali fedha na watu kufanikisha kazi nakuisaidia Serikali katika shughuli za kiuchumi na kijamii. Halmashauri itaendelea kutoa mazingira wezeshi kwa wadau kufanya shughuli zao ili kuifikia jamii nzima kwa kupitia Idara na Vitengo mbalimbali vilivyopo katika Halmashauri, Aidha, itaendelea kushirikiana na wadau waliopo na wengine watakaoendelea kujitokeza katika kuunga mkono Sera ya Maendeleo ya Jamii kuwawezesha jamii kuondokana na umasikini, kuwa na Afya bora, ustawi wa jamii na kuweza kujitegemea.

SEHEMU F: DAWATI LA JINSIA

UTANGULIZI:

Kitengo cha jinsia nimoja wapo ya vitengo vilivyo chini ya Idara ya Maendeleo ya Jamii ambacho kinafanya shughuli zake kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo ya serikali katika kuhakikisha jamiii inafikiwa katika masuala yote yahusuyo jinsia na maendeleo kwa ujumla wake;

MAJUKUMU YA KITENGO CHA JINSIA 

  • Kuratibu na kutoa ushauri kuhusu mambo yahusuyo masuala ya jinsia na kufuatilia uandaaji wa mpango wa jinsia kiwilaya.
  • Kuwa na kuweka takwimu muhimu zinazohusu jinsia na kuzifanyia kazi.
  • Kuhamasisha uanzishaji na uimarishaji wa vikundi vya kiuchumi.
  • Kuandaa mafunzo mbalimbali kwa jamii kiuhusu masuala ya jinsia na ujasiriamali.
  • Kuvipa usajili vikundi vya ujasiriamali vya kijamii.
  • Kusimamia utoaji na urejeshaji wa wamikopo ya vikundi vya wanawake.
  • Kuvisaidia vikundi namna ya kuchanganua miradi ya kiuchumi kwa kuzingatia masuala ya kijinsia.
  • Kuratibu na Kuandaa mafunzo mbalimbali kwa jamii/vikundi kuviwezesha kukua
  • Kiuchumi kwa kuwapa mikopo ya riba nafuu na kusimamia urejeshaji wa mikopo kwa wakati.
  • MAFANIKIO: 
  • Ongeza uelewa wa masuala ya jinsia kwa jamii hasa kupunguza unyanyasaji na umiliki wa mali kwa wanawake.
  • Upatikanaji wa huduma bora za kiuchumi na kijamii kuboreshwa katika jamii na vikundi vingi vya wanawake vimepatiwa mikopo na kuwafanya kuondokana na utegemezi na kupunguza umasikini.
  • Ongezeko la vikundi vya wanawake kujisajili na kujirasimisha na kufanya uzalishaji wenye viwango.

CHANGAMOTO:

  • Idara kukosa gari na hivyo kupelekea kushindwa kuyafikia maeneo mengi kwa wakati.
  • Vikundi vingi kutegemea shughuli za kilimo hivyo kushindwa kurejesha kwa wakati
  • Uchache wa mifuko hii hivyo kushindwa kuvifikia vikundi vingi kama vilivyoomba.
  • Maafisa m/jamii ngazi ya kata kukosa vyombo vya usafiri hivyo kushindwa kuwafikia wananchi walio wengi

SEHEMU G: KITENGO CHA VIJANA

UTANGULIZI

Kitengo cha Vijana kinatekeleza Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007, inayomtafsiri kijana ni mwenye umri kuanzia miaka 15-35. Katika kutekeleza Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007, Kitengo kimejidhatiti katika uwezeshaji wa kiuchumi, kutoa mafunzo, uhamasishaji na kutoa ushauri mbalimbali kwa vijana.

MAJUKUMU YA KITENGO CHA VIJANA

  • Kuwawezesha kiuchumi
  • Kuwawezesha Vijana kiuchumi kwa kuwapatia mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wa Wilaya(YDF) na wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wa Wizara
  • Uratibu na Uhamasishaji
  • Kuwa na kuweka takwimu muhimu zinazohusu Vijana na kuzifanyia kazi
  • Kuhamasisha vijana kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali na vikundi vya kuweka na kukopa na kujiunga na SACCOS)
  • Kuratibu, kufuatiliia na kutekeleza  shughuli za Vijana mfano, Vikundi vya uzalishaji mali, Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wa wilaya (YDF) na Wizarani
  • Kuratibu Mbio za mwenge wa Uhuru na Wiki ya Vijana
  • Kutoa ushauri wa kitaalam na kisheria wa masuala ya Vijana
  • Kuhimiza vijana katika shughuli za kujitolea
  • Kuvipa usajili vikundi vya ujasiriamali vya kijamii.
  • Kusimamia utoaji na urejeshaji wa wamikopo ya vikundi vya Vijana.
  • Mafunzo na Maendeleo ya Ujuzi
  • Kuandaa na kutoa mafunzo kwa Vijana katika masuala ya ujasiriamali,stadi za kazi, upangaji na uendeshaji wa miradi na uongozi
  • Kuandaa mafunzo ya kuwajengea uwezo Vijana  (capacity building)
  • Ushauri Nasaha Makuzi na Maongozi
  • Kutoa ushauri nasaha kwa vijana kuhusiana na masuala ya afya , stadi za maisha na elimu juu dhidi ya VVU na UKIMWI na dawa za kulevya
  • Kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa Vijana na stadi za maisha
  • Kutoa elimu ya maadili mema kwa Vijana ili waweze kujitambua na kuishi vizuri katika jamii
  • Kukuza dhana ya jinsia miongoni mwa vijana katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

MAFANIKIO: 

  • Upatikanaji wa huduma bora za kiuchumi na kijamii kuboreshwa katika jamii na vikundi vingi vya Vijana vimepatiwa mikopo na kuwafanya kuondokana na utegemezi na kupunguza umasikini.
  • Vijana wamewezeshwa kujitambua na kupewa mafunzo mbalimbali yahusiyo Vijana na maendeleo yao kwa ujuma ikiwemo ujasiriamali, Afya ya Uzazi, Stadi za Maisha, HIV/UKIMWI na elimu ya Jinsia.

CHANGAMOTO:

  • Idara kukosa gari na hivyo kupelekea kushindwa kuyafikia maeneo mengi kwa wakati.
  • Vikundi vingi kutegemea shughuli za kilimo hivyo kushindwa kurejesha kwa wakati
  • Fedha zilizotengwa kwa ajili ya kuwakopesha vijana ni ndogo kulinganisha na mahitaji ya Vijana wanaoomba mikopo
  • Kwa vijana ambao wamesoma wengi wao wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ajira
  • Vijana wengi hawako tayari kujitokeza kwenye mafunzo mbalimbali wakihisi kuwa wanapoteza muda, kwa kuwa mafunzo hayo hayana malipo (posho) kwao
  • Vijana wengi hawataki kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali kwa sababu vijana wengi hawana makazi maalumu hivyo kuishi kwa kuhamahama
  • Hakuna mazingira rafiki ya utoaji wa huduma za afya kwa vijana wa umri chini ya miaka 18 ambapo wanakuwa na hofu kuchanganyika na wenye umri mkubwa katika kupata huduma.

HITIMISHO

Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii itaendelea kutafuta rasilimali fedha kutoka vyanzo vingine vya mapato ili kuongeza nguvu ya utekelezaji wa shughuli zake kupitia vitengo vyake ili ifikie matokeo makubwa zaidi.

SEHEMU H: UJENZI NA UFUNDI

 MAJUKUMU YA KAZI YA KITENGO CHA KIKOSI CHA UJENZI NA UFUNDI

  • Kaufanya utafiti wa vifaa vya ujenzi na teknolojia zinavyopatikana katika Halmashauri
  • Kutoa uelewa na mafunzo ya teknolojia rahisi, sahihi na bunifu kwa jamii kuhusu ubunifu, uendeshaji na uenezaji wa vifaa vya ujenzi na teknolojia.
  • Kuwajengea jamii uwezo wa teknolojia rahisi, sahihi na banifu zilizofanyiwa utafiti kitaifa, Mkoa, Halmashauri na Asasi/Asiza zinazotambulika.
  • Kushiriki miradi mbalimbali inayotekezwa na jamii kama ujenzi wa shule, Zahanati, Marambo, Madaraja, Vivuko na Mifereji.
  • Kusanifu miundo, Madaraja, Kwenye jamii ili kuiwezesha jamuu hiyo kuwa na nyumba bora zenye gharama nafuu, vyoo bora na majiko sanifu
  • Kushirikiana na sekta zilizopo katika Halmashauri ili kuendeleza jamii.

MAFANIKIO

  • Kushirikiana na sekta zilizopo Halmashauri Sekta ya Elimu
  • Ujenzi wa maabara
  • Utengenezaji wa samani kwenye vyumba vya maabara Sekondari 4

Sekta ya ujenzi: Ukarabati wa madaraja mawili katika Kata ya Izyira

Sekta ya Afya

  • Utengenezaji wa samani (benchi 20, kabati 10, viti 24)
  • Kufanya makadirio ya milango 23 ya matundu ya vyoo 22 kati ya matundu hayo matundu mawili ni kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
  • Kuwajengea uwezo vikundi vya vijana 6 kwa ajili ya utengenezaji wa matofali ya udongo saruji

CHANGAMOTO

  • Kupopata usafiri na rasilimali fedha kwa wakati
  • Kuna mwitikio mdogo wa jamii kwa sababu miradi inatekelezwa kwa njia ya ukandarasi.
  • Ufinyu wa bajeti
  • Uhaba wa watumishi wa fani za bomba, uashi, umeme na umakenika.
  • Kazi za kijamii za kujitolea kupewa makandarasi.
  • Kitengo kuyumbishwa kuwa idara ya ujenzi au maendeleo ya jamii.
  • Kurukia magari ya Idara zingine na kutelezwa.

Njia zinazotumika kupambana na changamoto

  • Bajeti iongezwe kwenye kitengo
  • Miradi ya kijamii ifanyike na jamii husika, ili kuwe na umiriki na uendelevu
  • Watumishi waongezwe wenye fani husika
  • Mfumo wa kitengo uangaliwe na Halmashauri

Matangazo

  • VITUO VYA KUJIANDIKISHIA ORODHA YA WAPIGA KURA October 11, 2024
  • TANGAZO LA KAZI YA KUJITOLEA KWA KAZI YA MSAIDIZI WA WATOTO MAHAKAMANI February 02, 2022
  • TANGAZO LA ZOEZI LA UTOAJI WA ANWANIZA MAKAZI March 04, 2022
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA March 16, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • KIAPO CHA UTII KWA WAUGUZI MBEYADC

    May 16, 2025
  • BI. ERICA AMEMTEMBELEA ASKALI ALIELAZWA HOSPITALI YA IFISI

    May 08, 2025
  • Mapokezi ya Mhe Mchengerwa MbeyaDc

    April 26, 2025
  • Karibu Mhe. Mchengerwa

    April 25, 2025
  • Tazama zote

Picha Mwendo

"Wapo Wakuu wa Idara na Vitengo wakiamishwa watu wanafanya sherere" Waitara Naibu waziri TAMISEMI
Picha mwendo zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MBEYA

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti ya mkoa wa Mbeya

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

writingMasterThesis

Mahali

Wasiliana nasi

    Mbaliz Road

    Sanduku la posta: 599

    Simu ya mezani: 025-2502260

    Simu ya mkononi: 0762210758

    Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera binafsi
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma zetu

Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.