Halmashauri imepokea ujumbe kutoka Benki ya CRDB ulioongozwa na Bi. Faraja Kaziulaya, Meneja Mwandamizi wa Taasisi za Serikali kutoka CRDB Makao Makuu, aliyefika ofisini leo Septemba 17, 2025 kwa ajili ya kutoa shukrani kwa ushirikiano mzuri kati ya benki hiyo na Serikali.
Akizungumza katika kikao kifupi kilichohusisha wakuu wa idara na vitengo pamoja Bi. Kaziulaya amesema, kwa mara ya kwanza CRDB imeamua kutembelea wateja wake kwa lengo la kutoa shukrani badala ya kutangaza huduma zake kama ilivyozoeleka.
“Tumeona ni vyema kuwashukuru, kwani Serikali imekuwa mdau mkubwa kwa kutupatia zabuni mbalimbali za kutoa huduma za kifedha,” alisema.
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Bi. Erica E. Yegella, kaimu Mkurugenzi alimpa nafasi Bw. Mlungu kutoa salamu za shukrani kwa niaba ya Halmashauri, na kupongeza CRDB kwa kutambua mchango wa wateja wake.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.