Leo Agosti 27, 2025 Mkurugenzi Mtendaji, Bi Erica E. Yegella, amepokea ugeni maalum wa machifu kutoka Mkoani Ruvuma waliotembelea ofisi za Halmashauri kwa ziara ya mazungumzo na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya kijamii, utamaduni na maendeleo ya jamii.
Machifu hao wameongozwa na Chifu Akida Wabu Mtondo wa Pili, ambaye pia ni Katibu wa Machifu wa Kanda ya Kusini. Ziara hiyo imelenga kuimarisha ushirikiano baina ya viongozi wa kimila na taasisi za utawala rasmi katika kushughulikia changamoto za maendeleo na ustawi wa jamii.
Katika hotuba yake ya kuwapokea, Bi Yegella aliwapongeza machifu kwa nafasi yao muhimu katika jamii, hususan katika kutunza mila na desturi, pamoja na kuwa daraja kati ya wananchi na vyombo vya utawala.
“Nawakaribisha kwa mikono miwili. Machifu mmekuwa sehemu muhimu ya historia, utambulisho, na mshikamano wa jamii zetu. Ushirikiano kati yetu ni kichocheo cha maendeleo endelevu,” alisema Bi Yegella.
Kwa upande wake, Chifu Akida Wabu Mtondo wa Pili alieleza kufurahishwa kwake na mapokezi waliyoyapata, na kusisitiza umuhimu wa viongozi wa kimila kushirikiana kwa karibu na serikali na taasisi mbalimbali katika kuendeleza jamii.
“Tumefurahia sana mapokezi haya ya kipekee. Tunatarajia kuwa mazungumzo haya yatafungua milango zaidi ya ushirikiano kati ya viongozi wa kimila na taasisi zenu,” alisema Chifu Akida.
Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za kuimarisha nafasi ya viongozi wa kimila katika michakato ya maendeleo, huku ikitambua mchango wao wa kihistoria na kijamii katika kuleta mshikamano na amani katika maeneo wanayoyaongoza. Tunatarajia kuwa mazungumzo haya yatafungua milango zaidi ya ushirikiano kati ya viongozi wa kimila na taasisi zenu,” alisema Chifu Akida.
Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za kuimarisha nafasi ya viongozi wa kimila katika michakato ya maendeleo, huku ikitambua mchango wao wa kihistoria na kijamii katika kuleta mshikamano na amani katika maeneo wanayoyaongoza.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.