Serikali Mkoani Mbeya kupitia wakala wa barabara Tanzania TANROADS, imeanza kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan la kutengeneza barabara ya mchepuko katika eneo la Iwambi jijini Mbeya kuunganisha na Mbalizi ili kupunguza madhara yatokanayo na ajali za barabarani.
Ujenzi huo umeanza kutekelezwa na Wakala wa barabara Tanzania TANROADS Mkoa wa Mbeya akizungumza kwenye eneo unakofanyika utengezaji wa barabara hiyo katika kata ya Iwambi, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Beno Malisa, amesema tayari agizo hilo limeanza kufanyiwa kazi na TANROADS Mkoa wa Mbeya.
Kwa upande wake Meneja wa wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Mbeya Mhandisi Masige Matari, amesema tayari wameshafikisha vitendea kazi mbalimbali katika eneo la mradi na kuanza mara moja ujenzi wa barabara hiyo ikiwa ni pamoja na kuongeza upana wa barabara kuwa mkubwa zaidi ili kumudu magari makubwa kupishana.
Itakumbukwa mnamo Juni 07, 2025 huko katika eneo la Mbalizi mkoani Mbeya ilitokea ajali iliyosababisha umauti wa wananchi 28 na wengine tisa kujeruhiwa, ajali iliyohusisha magari matatu ambayo ni lori aina ya Scania lenye namba za usajili T. 830 EDP lenye tela namba T. 148 CTD, Coaster aina ya Mitsubishi Rosa lenye namba za usajili T. 257 DVP na gari lingine aina ya Toyota Lite Hiace lenye namba za usajili T. 185 DMF baada ya wa dereva wa lori aina ya Scania lenye namba za usajili T. 830 EDP lenye tela namba T. 148 CTD kuendesha gari kwa mwendokasi na kushindwa kulimudu gari lake hilo na hivyo kuyagonga magari mengine mawili.
Mbaliz Road
Postal Address: 599
Telephone: 025-2502260
Mobile: 0762210758
Email: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.