“Kwa kipindi hiki chondechonde badilisheni mwenendo kama mlikuwa mnajichanganya sana kwa kipindi hiki cha uchaguzi acha kabisa, tusije chafua sura ya tume ya uchaguzi “ Ndg.Stephen E Katemba.
Pia Katemba amewataka wasimamizi hao kuhakikisha wanafuata sheria, kanuni, taratibu, miongozo pamoja na maelekezo yanayotolewa na viongozi mbalimbali wakiwemo wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata.
Kauli hiyo imetolewa wakati wa zoezi la mafunzo na uapishaji wa wasimamizi wa uchaguzi wa vituo,wasimamizi wasaidizi, pamoja na makarani lililofanyika katika tarafa ya Tembela,Usongwe, na Isangati katika jimbo la Mbeya vijijini.
Mbaliz Road
Postal Address: 599
Telephone: 025-2502260
Mobile: 0762210758
Email: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.