• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Mbeya District Council
Mbeya District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Mbeya District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • Human Resources and Administration
      • Finance
      • Planning, Monitoring and Stastics
      • Health
      • Works
      • Water
      • Livestock and Fisheries
      • Community Development
      • Cleaning and Environment
      • Secondary Education
      • Agriculture, Irrigation and Cooperative
      • Primary Education
      • Land and Natural Resources
    • Units
      • ICT and Public Relations
      • Legal
      • Election
      • Internal Audit
      • Procurement Management
      • Bee keeping
  • Investment Opportunities
    • Tourists Attraction
    • Agriculture
    • Livestock
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
    • Expertise
  • Councilors
    • Councilors list
    • Standing Commitee
      • Finance, Administration and Planning Committee
      • Economics affairs, Construction and Environment Committee
      • Education, Health and Water Committee
      • AIDS Prevention Committee
    • Time table
      • Councilors Meetings
      • Visiting Chairperson
  • Projects
    • Approved Projects
    • On-going projects
    • Completed projects
  • Publications
    • By Laws
    • Service Contract
    • Strategic plan
    • Reports
      • Council Financial Report
      • Medium Term Expenditure Framework
      • Month Revenue and Expenditure Report
      • Council Development Report
      • Annual Performance and Financial Report
      • Full Council Minutes
    • Forms
    • Guidelines
      • Mwongozo wa Matumizi ya Vifaa vya TEHAMA
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

Halmashauri ya wilaya ya Mbeya imeokoa zaidi ya milioni 197 mahakamani

Posted on: May 4th, 2018

Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi 197,306,620/= baada ya kushinda kesi 5 katika mahakama mbalimbali nchini. Hayo yamebainishwa na mwanasheria wa halmashauri,  Wilson Nyamunda wakati akisoma taarifa ya kitengo cha sheria katika mkutano wa baraza la madiwani uliofanyika mei 4, 2018 kwenye ukumbi wa halmashauri.

Akizitaja kesi hizo Nyamunda amesema kesi ya kwanza ni ya madai ya makusanyo ya ushuru wa mazao kati ya halmashauri ya Wilaya ya Mbeya dhidi ya Thob Traders Ltd. Kesi Na. 9/2013 iliyokuwa mahakama kuu kanda ya Mbeya ambapo halmashauri imeshinda na kufanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi 118,000,000/=

Amesema kesi ya pili ni kesi Na. 103/2017 iliyokuwa baraza la ardhi na nyumba wilaya, kati ya Erick Mahenge na wenzake 66 wakiishitaki halmashauri kuwapandishia kodi ya pango katika vibanda vya biashara Mbalizi, kesi hii imefutwa na Halmashauri imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi 40,200,000/= zinazotokana na kodi hiyo.

Kesi ya tatu ameitaja kuwa ilikuwa tume ya usuluhishi wa migogoro kati ya Meshaki Kapange dhidi ya halmashauri ikiwa ni madai ya kusitishiwa mshahara kiasi cha shlingi 6,571,520/= kesi hii imetolewa uamuzi kwa tume kulitupilia mbali pingamizi la mlalamikaji.

Nyamunda ameitaja kesi ya nne kuwa ni kesi kati ya halmashauri dhidi ya Esthlajen Co. Ltd kesi ya madai Na. 36/2016 ikiwa ni madai ya makusanyo ushuru wa magulio kwa mwaka 2014/2015. Kiasi kinachodaiwa ni shilingi 13,035,100/= Nyamunda amesema kesi hii imeisha ambapo halmashauri imeshinda na sasa imeomba nakala ya hukumu na mwenendo wa kesi kwa ajili ya kukaza hukumu.

Pia ameitaja kesi ya tano kuwa ni kesi ya madai Na. 45 kati ya Halmashauri dhidi ya Obadia Haruna ikiwa ni madai ya ushuru wa stendi Mbalizi kiasi cha shllingi 19,500,000/=

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya, Mhe. Mwalingo Kisemba amewapongeza wataalamu wa halmashauri hususani kitengo cha sheria kwa kuiongoza halmashauri kushinda kesi hizo na kuisadia kuokoa kiasi hicho cha fedha.

Aidha Mhe. Kisemba amesema kuwa kesi nyingi zilizokuwa zinaikabili halmashauri zimetokana na madai ya ushuru ikiwa imesababishwa na mawakala kutowasilisha ushuru huo kwa wakati. Hivyo amesema kwa sasa halmashauri imejipanga kutozalisha kesi hizo kwa sababu sasa halmashauri inakusanya yenyewe ushuru huo bila ya kutumia mawakala kama ilivyokuwa awali.

“lakini pia huko nyuma tulikuwa tunafanya kazi na mawakala sasa hivi tunakusanya mapato wenyewe na tumeona mafanikio ya kutosha. Halmashauri yetu inamaeneo mengi ya kuzallisha nadhani tukijikita kuhakikisha kila ushuru unaopaswa kutolewa utakuwa unatolewa hatutafika tena mahakamani”

Naye diwani wa viti maalumu, Mhe. Aida Haule amesema kuwa halmashauri kwa kushinda kesi hizo imesaidia kuokoa pesa ambazo zitatumika kukamilisha  miradi mbalimbali ya maendeleo iliyosimama kutokana na ukosefu wa fedha ikiwemo miradi ya elimu, afya na maji.

Announcements

  • VITUO VYA KUJIANDIKISHIA ORODHA YA WAPIGA KURA October 11, 2024
  • TANGAZO LA KAZI YA KUJITOLEA KWA KAZI YA MSAIDIZI WA WATOTO MAHAKAMANI February 02, 2022
  • TANGAZO LA ZOEZI LA UTOAJI WA ANWANIZA MAKAZI March 04, 2022
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA March 16, 2022
  • View All

Latest News

  • CRDB BENKI YATOA SHUKRANI KWA WATEJA WA HALMASHAURI

    September 17, 2025
  • RC MBEYA AHIMIZA MATUMIZI NISHATI SAFI.

    August 29, 2025
  • DC ITUNDA AKUTANA NA MACHIFU WA HALMASAHAURI YA WILAYA YA MBEYA

    August 28, 2025
  • DED ERICA E. YEGELLA APOKEA UGENI WA MACHIFU KUTOKA MKOA WA RUVUMA

    August 27, 2025
  • View All

Video

"Wapo Wakuu wa Idara na Vitengo wakiamishwa watu wanafanya sherere" Waitara Naibu waziri TAMISEMI
More Videos

Quick Links

  • MBEYA

Related Links

  • Ikulu
  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti ya mkoa wa Mbeya

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Mbaliz Road

    Postal Address: 599

    Telephone: 025-2502260

    Mobile: 0762210758

    Email: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.