Matukio katika picha wakati Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe Mohamed Mchengerwa alipowasili katika shule ya Sekondari Lwanjilo aambapo ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa unaoendelea wa vyumba vinne vya madarasa ya kidato cha tano na sita katika Kata ya Lwanjilo.
Mhe Mchengerwa ameweka jiwe la Msingi hapo jana katima sikukuu ya Muungano ambayo kimkoa ilifanyika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
Aidha Mhe Waziri amempongeza Mkurugenzi Mtendaji Bi Erica E Yegella kwa usimamizi mzuri wa miradi inayoletwa na Serikali ya awamu ya sita.
Mhe Mchengerwa ameahidi kufikia June 30, 2025 vifaa vya tehama vitakuwa vimefika shuleni hapo kwa ajili ya wananfunzi kujifunzia. Akimuelekeza Mkurugenzi msaidizi wa Elimu Maalum na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi
ndugu Ernest X Hinju. Kufuatia ombi la Mhe Diwani wa Kata ya Lwanjilo.
Mbaliz Road
Postal Address: 599
Telephone: 025-2502260
Mobile: 0762210758
Email: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.