Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya wilaya ya Mbeya Ndg. Stephen E. Katemba amewataka maafisa Elimu wa wilaya na kata kuhakikisha wanawasimamia wanafunzi kuimba nyimbo kuu tatu za taifa.
Hayo yamesemwa wakati wa kikao na Maafisa elimu wa wilaya na kata kilicho fanyika katika ukumbi halmashauri ya wilaya ya Mbeya chenye lengo la kuwakumbusha maafisa hao juu ya agizo la serikali la kusimamia utekelezaji wa uimbaji wa nyimbo kuu tatu za Tanzania.
Katemba amesema kuwa kila mtu ajue kuwa anawajibu wa kusimamia na kuhakisha kuwa nyimbo hizo zinaimbwa katika maeneo yake kwani nyimbo hizo zina maana kubwa kwani zinawafundisha wanafunzi uzalendo na kuwakumbusha misingi mikuu ya nchi yetu.
“ maelekezo ya namna hii kila mtu atimize wajibu wake kitendo cha kukaidi maagizo yanayo tolewa na viongozo ni utovu wa nidhamu uimbaji wa nyimbo hizo si kwa shule za serikali peke yake ni pamoja na shule binafsi, mim nimesha tekeleza langu na sitegemei kupita katika maeneo yenu ya shule nikute watoto wanaruhusiwa kuingia madarasani bila kuimba nyimbo hizo ” Katemba.
Nyimbo hizo kuu tatu ni pamoja na tazama ramani, Tanzania –tanzania na Mungu ibariki Tanzania ambazo hata maafisa elimu hao waliweza kujikumbusha kwa kuimba mbele ya mkurugenzi.
Mbaliz Road
Postal Address: 599
Telephone: 025-2502260
Mobile: 0762210758
Email: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.