MSLAC YAMALIZA MGOGORO WA SHAMBA KATA YA LWANJILO MBEYA DC.
Timu ya wataalamu na wanasheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wanao tekeleza kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia legal aid, wamemaliza mgogoro wa shamba ulio dumu kwa zaidi ya mwaka mmoja kati ya mzee Benson Malidadi na Fred Saimon wote wakazi wa kijiji cha ilowelo kata ya Lwanjilo halmashauri ya wilaya ya Mbeya.
Mapema hii leo mzee Benson Malidadi aliwasilisha malalamiko ya mgogoro wake kwenye timu hiyo ya wataalamu akimlalamikia bwana Fred Saimon kwa kuuza shamba lake bila kumtaalifu zaidi ya mwaka mmoja uliopita, ambapo timu hiyo imesuruhisha mgogoro huo kwa makubaliano maalum kati ya wazee hao.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.