Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Bi. Erica Yegella akiwa ameongozana na Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt Hamadi Mwalukunga. leo hii ametembelea Hospitali ya Mbalizi-Ifisi ambapo alifika kwa lengo la kumjulia hali Askari Polisi aliyelazwa katika wodi binafsi baada ya kuugua ghafla akiwa kazini.
Sambamba na hilo Bi. Yegella alipata wasaa wa kufanya mazungumzo mafupi na Viongozi wa Hospitali wakiongozwa na Mganga Mfawidhi Msaidizi Dkt. Khamisi Bakari Ally, Katibu wa Afya Bi. Faustina Fanuel Mahenge na Mhasibu Ndg. Gabriel Gwakisa.
Mazungumzo hayo lililenga hasa kukuza na kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya na Hospitali ya Mbalizi katika utoaji wa Huduma za kiafya.
Vilevile Bi. Yegella aliupongeza Uongozi wa Hospitali kwa kazi nzuri alisisitiza kuwa Serikali iko pamoja na Hospitali katika kila jambo na kuwaomba Watumishi kuendelea kutoa Huduma bora za kiafya kwa wananchi wote wa Halmashauri.
Ikumbukwe kuwa baadhi ya watumishi wa Afya wakiwemo Madaktari na wauguzi wanaofanya kazi katika Hospitali ya Mbalizi-Ifisi ni waajiriwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.