Katibu tawala msaidizi wa Mkoa wa Mbeya CPA Edward Malima ameipongeza Halmashauri ya Mbeya DC kwa kufanikisha ukusanyaji mzuri wa mapato uliofikia asilimia 71% kwa mwaka 2024-2025.
‘’ Kwenye upande wa ukusanyaji mapato ya ndani kwakweli mnafanya vizuri hadi mwezi December 31, 2024 mlikuwa asilimia 59 kwa maana Jola lengo kwa asilimia 9 na taarifa ya sasa niliyonayo January 24,2025 mko asilimia 71 hii nikutokana na uwongozi wako Mh.Mwenyekiti na waheshimiwa madiwani na ushirikiano na management ndiyo maana umefika hapa maelekezo yenu yanazingatiwa vizuri kwa upande wa mapato nawapongezeni sana tunaona jitihada zenu mnazozifanya,lakini kwenye eneo hili tuombe tuzingatie taratibu za Serikali kutenga asilimia 40 kwaajili ya miradi ya maendeleo tusije tukasahau’’.Amesema Malima
Katika hatua nyingine Malima ameeleza dhamira yake yakuhakikisha ujenzi wa Barabara inayo unganisha Mbeya mpaka Njombe kupitia Isyonje hadi Kikondo yenye urefu wa kilomita 22 unakamilika kwa haraka na kusema kuwa ukamilikaji wa Barabara hiyo utatoa fursa kubwa ya ukuaji wa kiuchumi ndani ya mkoa wa Mbeya.
Mwenyekiti wa kikao hicho Mwalyigo Kisenga ameahidi kutoa ushirikiano mzuri kwa Mkurugenzi mpya Mheshimiwa Erica Yegella ilikuhakikisha kwamba Halmashauri ya Mbeya DC inazidi kukua na kutoa huduma bora kwa wananchi.
‘’Amesimamia vizuri pamoja na mambo mengine Mama ukitaka kwenda na sisi kama utamuliza huyo atakwambia siri yetu wala usipate shida kwamaana angekuwa amehama ungepata shida lakini huku hakuna ugumu wowote nikushirikiana tu kwakweli kwa uwazi wala hakuna kitu kigumu kabisa baada ya kusema hayo sasa nilikuwa najaribu kupokea niliyo ambiwa na wakubwa zetu pamoja na Mkurugenzi wetu tunakukaribisha uzuri unatimu yote ya watumishi ambayo kama unayoona hayo mapato siyo Mapunda pekeyake ni management nzima wanajua siri ya kufanya vizuri we shirikiana nao sisi utatuona kwenye vikao tu lakini utakao kuwanao kila siku ni hawa ndiyo wanaojua kila kitu kilivyo kuliko hata sisi’’Amesema Kisenga.
Kwa upande mwingine Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ametoa ufafanuzi kwa fedha zote zilizo patikana katika Halmashauri hii zitatumika kama zilivyo pangwa.
‘’Lakini tunaahidi fedha zote zitatumika ipasavyo na leo nimeanza kazi na kazi kwenye Bilioni moja ya hapa hapa kwenye kata yetu ya Iwindi kwenye hili jengo la Halmashauri hiyo bilioni moja imeletwa kwaajili ya vitu vitatu cha kwanza Uzio wa Jengo hili la Halmashauri cha pili Cafetaria na chatatu ni landscaping ilikuonyesha sura na taswira ya Jengo letu liwe na kuvutiwa na kuonyesha kuwa serikali iko hapa katika Halmashauri ya wilaya ya Mbeya’’ Amesema Yegella.
Pongezi na maamuzi hayo yanaonyesha dhamira ya viongozi wa Halmashauri ya Wilaya Mbeya katika kuimarisha maendeleo na ustawi wa kijamii huku wakisisitiza umuhimu wa jamii kushirikiana na Serikali katika kuitumia vyema rasilimali na miundo mbinu iliyopo.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.