Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe Solomoni Itunda leo Julai 26, 2025 ameongoza kamati ya ulinzi na usalama kukagua miradi itakayopitiwa na mwenge wa Uhuru 2025 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Miradi ilokaguliwa ni pamoja na madarasa matatu na matundu nane katika sshule ya Sekondari Ihango, Jengo la kutunzia hewa ya oxygen katika hospitali ya Wilaya, matumizi ya nishati safi katika chuo cha maendeleo ya jamii, daraja pamoja na mradi wa Maji uliopo Kata ya Inyala.
Mhe Itunda amempongeza Mkurugenzi pamoja na Menejimenti kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo iloletwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wake Dkt Samia Suluhu Hassan.
Aidha amewataka wananchi na watumiaji wa miradi hiyo kuitumia kwa uzuri ili iweze kudumu kwa muda mrefu.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.