Katika juhudi za kuendelea kutangaza fursa za uwekezaji na ukuzaji uchumi wa wananchi, mashirika binafsi na Serikali kwa ujumla wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Bi. Erica Yegella, amekutana na uongozi wa benki na NMB tawi la Usongwe mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi wilayani Mbeya na kuwataka kuendeleza ushirikiano na Halmashauri ili kuimarisha uchumi wilayani humo.
Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya Mbeya amekuwa na utaratibu wa kukutana na kampuni mbalimbali za binafsi na zile za Serikali kwa lengo kuu la kuendelea kuimarisha ushirikiano, kufahamiana na kueleza fursa zilizopo wilayani Mbeya kulingana shughuli ambazo wadau husika wanakuwa wanajishusisha nazo.
Benki ya NMB hasa katika tawi lake la Usongwe Mbalizi ina uwanda mpana wa kutanua huduma yake kupitia mawakala na kufika vijijini ili kuimarisha uchumi wa wananchi kupitia mikopo na fursa mbalimbali ikiwemo kwenye maeneo ya kilimo, biashara na ufugaji wilayani Mbeya ili kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na Serikali kwa ujumla kupitia ziara hiyo ya mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mbeya ambapo uongozi wa benki hiyo umeshukuru kwa kiongozi huyo kuwatembelea katika kuendelea kuimarisha mshkamano kwenye utoaji huduma kwa jamii na kauli mbiu yao 'NMB karibu yako'.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.