• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za watumishi |
Mbeya District Council
Mbeya District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya Mbeya

  • Nyumbani
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mifugo na uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA na Mahusiano
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi
      • Ufugaji wa nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Wataalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
      • Taarifa ya fedha
      • Mpango wa Mapato na Matumizi
      • Mapato na Matumizi ya Mwezi
      • Taarifa ya miradi ya maendeleo
      • Taarifa ya fedha ya mwaka
      • Mihtasari ya Mikutano ya Baraza
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
      • Mwongozo wa Matumizi ya Vifaa vya TEHAMA
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Picha mwendo
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

DED YEGELLA: FEDHA ZA NDANI KUNUFAISHA KATA ZOTE MBEYA DC

Imewekwa: February 10th, 2026

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya (Mbeya DC), Bi. Erica Yegella, amesema kuwa mapato yote yatakayokusanywa kutoka katika vyanzo vya ndani vya Halmashauri yatatumika kugharamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kata zote 28 za wilaya hiyo.

Bi. Yegella ameyasema hayo leo wakati wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Halmashauri ya Wilaya (DCC), kilichoketi kujadili na kupitisha Rasimu ya Mapendekezo ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027.

Ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha huo, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imepanga kukusanya na kutumia jumla ya shilingi bilioni 72.4 kutoka vyanzo mbalimbali, ikiwemo mapato ya ndani na ruzuku kutoka Serikali Kuu. Fedha hizo zitagharamia mishahara, matumizi ya kawaida (OC), utekelezaji wa miradi ya maendeleo, pamoja na vyanzo fungiwa kama 'CHF', 'User Fee', 'NHIF' na Michango ya Jamii.

Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema Watendaji wa Kata (WEOs) na Watendaji wa Vijiji (VEOs), kwa kushirikiana na viongozi wengine wa kata na vijiji wakiwemo Wenyeviti wa Vijiji na Madiwani, wamefanya kazi kubwa katika kuhakikisha malengo ya ukusanyaji wa mapato ya ndani yanafikiwa kama ilivyopangwa.

Aidha, ameongeza kuwa kupitia ushirikiano wa pamoja, Halmashauri imefanikiwa kudhibiti utoroshwaji wa mazao, ikiwemo kukamata magunia yaliyofungwa kwa mtindo haramu wa lumbesa yakitoka Halmashauri tunazopakana nazo.

“Kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, tumeweza kukamata na kutoza faini mizigo iliyofungwa kwa mtindo haramu wa lumbesa kwa asilimia 228. Vilevile, mchakato wa uuzaji wa viwanja vya Tanganyika Packers umefikia asilimia 850, huku makusanyo ya vibali vya ujenzi yakifikia asilimia 14,” amesema Bi. Yegella.

Akisisitiza kuhusu fedha za miradi ya maendeleo, Bi. Yegella amesema kuwa mapato ya ndani yatapelekwa moja kwa moja kwenye kata husika. Mpango uliopo ni kuhakikisha kila kata inapatiwa shilingi milioni 5, huku kipaumbele kikielekezwa kwenye kata ambazo hazijawahi kunufaika na fedha hizo hapo awali.

Ameongeza kuwa Halmashauri inaendelea kuimarisha mawasiliano na ufuatiliaji ili kuhakikisha kila fedha inayotolewa inatumika kikamilifu kwa lengo lililokusudiwa, kwa manufaa ya wananchi wa Wilaya ya Mbeya.

Matangazo

  • VITUO VYA KUJIANDIKISHIA ORODHA YA WAPIGA KURA October 11, 2024
  • TANGAZO LA KAZI YA KUJITOLEA KWA KAZI YA MSAIDIZI WA WATOTO MAHAKAMANI February 02, 2022
  • TANGAZO LA ZOEZI LA UTOAJI WA ANWANIZA MAKAZI March 04, 2022
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA March 16, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MBEYA DC YASISITIZA MATUMIZI SAHIHI MIKOPO YA ASILIMIA 10

    February 11, 2026
  • RPC MBEYA AMKABIDHI CHETI CHA SHUKRANI MKURUGENZI MTENDAJI MBEYA DC

    February 11, 2026
  • DC ITUNDA AWAAGIZA WEOs NA VEOs KUSIMAMIA MPANGO WA CHAKULA SHULENI

    February 10, 2026
  • DED YEGELLA: FEDHA ZA NDANI KUNUFAISHA KATA ZOTE MBEYA DC

    February 10, 2026
  • Tazama zote

Picha Mwendo

"Wapo Wakuu wa Idara na Vitengo wakiamishwa watu wanafanya sherere" Waitara Naibu waziri TAMISEMI
Picha mwendo zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MBEYA

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti ya mkoa wa Mbeya

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

writingMasterThesis

Mahali

Wasiliana nasi

    Mbaliz Road

    Sanduku la posta: 599

    Simu ya mezani: 025-2502260

    Simu ya mkononi: 0762210758

    Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera binafsi
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma zetu

Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.