• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za watumishi |
Mbeya District Council
Mbeya District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya Mbeya

  • Nyumbani
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mifugo na uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA na Mahusiano
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi
      • Ufugaji wa nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Wataalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
      • Taarifa ya fedha
      • Mpango wa Mapato na Matumizi
      • Mapato na Matumizi ya Mwezi
      • Taarifa ya miradi ya maendeleo
      • Taarifa ya fedha ya mwaka
      • Mihtasari ya Mikutano ya Baraza
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
      • Mwongozo wa Matumizi ya Vifaa vya TEHAMA
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Picha mwendo
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Halmashauri Imezindua Mpango Mkakati wa Elimu wa Mwaka 2018

Imewekwa: October 31st, 2017

Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imezindua mpango Mkakati wa elimu kwa shule za msingi wenye  lengo la kuinua ufaulu kutoka asilimia 61.4 ya mwaka 2017 hadi asilimia 93 kwa mwaka 2018. Akizindua mpango mkakati huo Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya, Ndg, Hassan Mkwawa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa kuzigeuza  changamoto zinazozikabili Idara ya Eliumu kuwa ni fursa na hatimaye kuja na mpango mkakati huo.

“Kumekuwa na changamoto nyingi ambapo wameamua changamoto hizo kuzigeuza kuwa malengo, na ni chukue fursa hii sasa kuwapongeza kwa sababu tungeendelea kuzichukulia hizi kama ni changamoto tusingekuja na mpango maalumu wa kuja kuinua kiwango cha ufaulu katika shule zetu”

Ndg. Mkwawa amesema kuwa ili malengo ya mkakati huo yaweze kufikiwa ni lazima Halmashauri iusimamie ipasavyo na kuhakikisha kila mdau anatekeleza majukumu yake ipasavyo.

Ndg. Mkwawa amezindua mpango mkakati huo kwenye kikao cha wadau wa elimu kilichoandaliwa na idara ya elimu msingi. Wadau waliohudhuria katika kikao hicho ni pamoja na wenyeviti wa vijij, watendaji wa vijiji, watedaji kata, waheshimiwa madiwani, walimu wakuu, maafisa elimu kata, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wazazi, taasisi za fedha, taasisi za kiraia na wazazi.

Awali akiwasilisha mpango mkakati huo ili uweze kujadiliwa, Afisa Elimu Msingi Wilaya, Mwl. Vicent Kayombo amesema kuwa mpango mkakati huo unaitwa Mpango Mkakati wa Elimu wa Isuto wa mwaka 2018. Amesema umepewa jina la Isuto kwa sababu shule ya mwisho kiwilaya inatoka kata ya Isuto, na kuitaja shule hiyo kuwa ni Shule ya Msingi Shitete ambayo haikufaulisha hata mwanafunzi mmoja kati ya wanafunzi 36 waliofanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi.

Pia Mwl. Kayombo amesema kuwa mpango mkakati huo umewasilishwa kwa wadau wa Halmashauri nzima ili waweze kuufahamu na kuwa na lengo moja kwani suala la ufaulu wa wanafunzi si suala la kuachiwa walimu pekeyao au idara ya elimu peke yake. Amesema kwa kutambua hilo ndio maana mpango mkakati huo umebeba kauli mbiu inayosema kuwa “Ufaulu wa Juu ni Ushirikiano wa Mimi na Wewe”

Vile vile amesema kuwa mpango mkakati huo umewasilishwa kwa wadau ili weweze kuujadili na kuuelewa kisha kuupeleka kwa wananchi kuutekeleza kwa pamoja, kwani wakiulewa wao kama viongozi itakuwa ni rahisi kutekelezwa.

“Leo sasa mpango huu, umeletwa mbele ya  wadau wa elimu, wadau wa elimu ambao  ni viongozi ili nao waweze kuupitia, kuachambua, ili maazimio yake, yatakuwa sasa ndio dira ya kushuka kule chini kwa wananchi. Idara ya Elimu Msingi inaamini kwamba wananchi wako tayari, wazazi wako tayari, tatizo ni sisi viongozi. Viongozi tukiwa na uelewa wa pamoja tukashusha maelekezo, tukawa mfano kule chini, tunaamini wazazi watatuunga mkoni kikamilifu, na hatimaye tutafikia malengo ambayo tumejiwekea.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. Ntokani akifunga mjadala baada ya wadau kuujadili na kuukubali mpango mkakati huo amesema kuwa kilichobaki sasa ni kufanya kwa vitendo. Na kuwaomba wadau kudumisha mshikamano na ushirikiano katika kutatua changamoto za elimu na kuzigeuza kuwa fursa kama mpango mkakati ulivyoelezea ili lengo liweze kufikiwa.

“naomba sana tujitahidi, baada ya kutoka hapa twende tukafanye kazi ya kushikana na kushikamana kwa kuhakikisha tunaziondoa hizo changamoto zilizopo kwenye maeneo yetu”

Matangazo

  • VITUO VYA KUJIANDIKISHIA ORODHA YA WAPIGA KURA October 11, 2024
  • TANGAZO LA KAZI YA KUJITOLEA KWA KAZI YA MSAIDIZI WA WATOTO MAHAKAMANI February 02, 2022
  • TANGAZO LA ZOEZI LA UTOAJI WA ANWANIZA MAKAZI March 04, 2022
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA March 16, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • KIAPO CHA UTII KWA WAUGUZI MBEYADC

    May 16, 2025
  • BI. ERICA AMEMTEMBELEA ASKALI ALIELAZWA HOSPITALI YA IFISI

    May 08, 2025
  • Mapokezi ya Mhe Mchengerwa MbeyaDc

    April 26, 2025
  • Karibu Mhe. Mchengerwa

    April 25, 2025
  • Tazama zote

Picha Mwendo

"Wapo Wakuu wa Idara na Vitengo wakiamishwa watu wanafanya sherere" Waitara Naibu waziri TAMISEMI
Picha mwendo zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MBEYA

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti ya mkoa wa Mbeya

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

writingMasterThesis

Mahali

Wasiliana nasi

    Mbaliz Road

    Sanduku la posta: 599

    Simu ya mezani: 025-2502260

    Simu ya mkononi: 0762210758

    Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera binafsi
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma zetu

Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.