• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za watumishi |
Mbeya District Council
Mbeya District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya Mbeya

  • Nyumbani
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mifugo na uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA na Mahusiano
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi
      • Ufugaji wa nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Wataalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
      • Taarifa ya fedha
      • Mpango wa Mapato na Matumizi
      • Mapato na Matumizi ya Mwezi
      • Taarifa ya miradi ya maendeleo
      • Taarifa ya fedha ya mwaka
      • Mihtasari ya Mikutano ya Baraza
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
      • Mwongozo wa Matumizi ya Vifaa vya TEHAMA
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Picha mwendo
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imetekeleza ahadi yake ya kutoa mikopo kwa wanawake na vijana kila baada ya miezi mitatu

Imewekwa: March 22nd, 2018

Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, imeendelea kutekeleza ahadi yake ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana kila baada ya miezi mitatu. Ahadi hiyo imetekelezwa baada ya kutoa mkopo wa fedha wenye thahamani ya shilingi milioni 70.5 kwa vikundi 13 vya wanawake na vikundi viwili vya vijana.

Akikabidhi mkopo huo Kaimu Afisa Tawala Wilaya Ndg. Aron Sote kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Mhe. Poul Ntinika ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa kutekeleza ahadi yake kwa vitendo. Mbali na kuipongeza Halmashauri, pia  Sote ameitaka Halmashauri kufuatilia kwa ukaribu fedha hizo kwa wanavikundi ili kuhakikisha lengo waliloliombea fedha hizo linafikiwa.

“Nimshukuru Mkurugenzi na timu yake na Mwenyekiti wa Halmashauri  kwa kuwajali wanawake. Lakini Mkurugenzi niombe hawa ambao leo hapa tumetoa mikopo tumewapa ni vyema tuwafualie kwa ukaribu. Maana hapa kwenye ratiba naona wote kilimo, ufugaji sijui nini ni vyema tukaenda kuona hali halisi, hivi wanavyosema viazi ni kweli je wamelima?  Au wanatuweka changa la mawe hapa ili ionekane wanalima viazi kumbe wakifika nyumbani hizi hela wanagawana. Baadae inakuwa shida kuzirudisha”

Vilevile Ndg. Sote amewaambia wanavikundi wazitumie pesa hizo vizuri kwani fedha walizopewa ni mikopo na wanapaswa kuzirudisha ili ziweze kusaidia watu wengine.

“Hizi hela ni endelevu zinatoka kwenu zinaenda kwa wengine tena. Niwahase nyie mliopata hizi hela zitumieni kwenye malengo ambayo mmeombea Halimashauri, kuna mwaka Fulani niliona wameandika andiko vizuri, wamejihoredhesha majina lakini baadae tunaenda kudai zile hela inaonekana mwenyekiti na mtendaji basi. Sijui kama na hili mmeliona kama lipo naomba lizibitiwe. Wapewe walengwa kabisa na nyinyi walengwa zitumieni hizi hela kwa malengo ambayo mnayo”

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Ndg. Zena Kapama amesema, Halmashauri imeweka mkakati unayoibana Halmashauri hiyo kutoa mikopo hiyo kila robo, tofauti na hapo awali ambapo ilikua inatoa kwa mkupuo. Amesema lengo la Halmashauri kuweka mkakati huo ni kuiwezesha kutekeleza kwa urahisi  matakwa ya sera ya nchi inayotaka Halmashauri zote nchini kutenga asilimia kumi ya makusanyo kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana.

Mkakati huo uliwekwa na Halmashauri mwezi Oktoba, 2017. Ambapo mpaka sasa jumla ya shilingi milioni 244.5 zimetolewa kwa vikundi 61 vya wanawake na vijana. Kati ya vikundi hivyo vikundi 44 ni vya wanawake na vikundi 17 ni vya vijana. Vikundi vya wanawake vimekopeshwa jumla ya shilingi milioni 181.5 na vijana vimekopeshwa jumla ya shilingi milioni 63. Fedha hizo zimekopeswa na Halmashauri kwa awamu tatu za robo ya mwaka wa fedha 2017/2018.

“Mhe. Mgeni rasmi Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya inamkakati wa kutoa mikopo kila robo kuanzia mwaka huu wa fedha 2017/2018 na mikopo hii inayotolewa leo inatolewa ikiwa ni ya awamu ya tatu ya mwaka huu wa fedha”. Amesema Ndg.Kapama

Matangazo

  • VITUO VYA KUJIANDIKISHIA ORODHA YA WAPIGA KURA October 11, 2024
  • TANGAZO LA KAZI YA KUJITOLEA KWA KAZI YA MSAIDIZI WA WATOTO MAHAKAMANI February 02, 2022
  • TANGAZO LA ZOEZI LA UTOAJI WA ANWANIZA MAKAZI March 04, 2022
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA March 16, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MIKOPO SIO ZAWADI, NI YA MAENDELEO.

    July 03, 2025
  • DC MBEYA AFUATILIA AGIZO LA RC HOMERA UJENZI WA BARABARA YA MCHEPUKO IWAMBI MBALIZI, ARIDHISHWA NA KASI YAKE.

    June 10, 2025
  • Tuheshimu Sheria na taratibu zilizowekwa na Serikali- DED Erica..

    June 06, 2025
  • MbeyaDc yaadhimisha siku ya Mazingira Duniani kwa kufanya usafi katika Mto Mbalizi

    June 05, 2025
  • Tazama zote

Picha Mwendo

"Wapo Wakuu wa Idara na Vitengo wakiamishwa watu wanafanya sherere" Waitara Naibu waziri TAMISEMI
Picha mwendo zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MBEYA

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti ya mkoa wa Mbeya

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

writingMasterThesis

Mahali

Wasiliana nasi

    Mbaliz Road

    Sanduku la posta: 599

    Simu ya mezani: 025-2502260

    Simu ya mkononi: 0762210758

    Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera binafsi
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma zetu

Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.