• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za watumishi |
Mbeya District Council
Mbeya District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya Mbeya

  • Nyumbani
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mifugo na uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA na Mahusiano
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi
      • Ufugaji wa nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Wataalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
      • Taarifa ya fedha
      • Mpango wa Mapato na Matumizi
      • Mapato na Matumizi ya Mwezi
      • Taarifa ya miradi ya maendeleo
      • Taarifa ya fedha ya mwaka
      • Mihtasari ya Mikutano ya Baraza
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
      • Mwongozo wa Matumizi ya Vifaa vya TEHAMA
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Picha mwendo
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Imetoa mkopo wa Milioni 174 kwa vikundi 46 vya Wanawake na Vijana

Imewekwa: October 6th, 2017

Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imetoa mkopo wa Shilingi Milioni 174 kwa vikundi 46 vya wanawake na vijana. Kati ya vikundi hivyo vilivyopata mkopo vikundi 31 ni vya wanawake ambavyo vimepata mkopo wenye thamani ya Shilingi Milioni 121, na vikundi 15 ni vya vijana vilivyopatiwa mkopo wa Shilingi Milioni 53.

Akikabidhi mkopo huo kwa walengwa Mkuu wa Wilaya ya  Mbeya, Mhe. Willium Paul Ntinika ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa kutekeleza agizo la Serikali linalozitaka Halmashauri zote nchini kutenga asilimia kumi (10%) ya mapato yake kila mwaka kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanawake na vijana.

“Nitoe shukurani zangu za dhati kuipongeza Halmashauri, nimpongeze Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na Mkurugenzi Mtendaji kwa kuendelea kutekeleza agizo la serikali, hongereni sana”

Pia Mhe. Ntinika amewataka wanavikundi waliopata mikopo hiyo kuitumia kwa tija ili lengo lililowekwa na Serikali katika kutoa mikopo hiyo liweze kufukiwa. Mhe. Ntinika amesema mikopo waliyopewa si zawadi bali wamepewa kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi na watalazimika kuirejesha baada ya kuisha siku thelathini ili wananchi wengine waliokosa mikopo hiyo awamu hii waweze kupata katika awamu zinazofuata.

 “Pia naomba kuchukua fursa hii kuwapongeza wanavikundi mliobahatika kupata mikopo hii kwa siku hii ya leo kwa sababu nina amini kuna wengi waliomba lakini nyie mpata bahati hii kwa hiyo bahati hii muitumieni vizuri. Nina amini mikopo hii inayokuja kwenu itafanye kazi iliyokusudiwa kwa sababu mmeandika kusudio la kuomba mkopo,  mkopo huo uende sambamba na kile ambacho mlichokusidia, laniki mkumbuke kurejesha. Nilifundisha mwaka jana kwamba ukipewa mkopo pige hesabu yako kwaba kila mwezi unatakiwa kurudisha shilingi ngapi, unaziandika muda ukifika unarudisha. Hivyo basi matarajio yangu ni kwamba mikopo hii mtaanza kurejesha baada ya kuisha siku 30”

Licha ya kuwasisitiza wanavikundi kurejesha pesa walizokopa kwa wakati, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Mhe. Kisemba Mwalingo amewataka wanavikundi hao kuwa wabunifu katika kufanya kazi zao ili kufikia uchumi wa viwanda kwa kuanzisha viwanda vidogo ili kumuunga mkono Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kauli mbiu yakwe inayosema Tanzania ya viwanda.

“kwa bahati mbaya sana Rais anaposema Tanzania ya Viwanda watu wandani hii ni ndoto isiyotekelezeka kwa sababu hawajui ni ni maana ya kiwanda, hawajui kwamba kunaviwanda vikubwa, vya kati na vidogo. Naomba muelewe kwamba kiwanda ni kubadilisha malighafi kwenda katika kutumika.  Kwamba kama ilikua pamba izae nguo, kama yalikua maembe yazae juisi. kinachofanya hivyo ni kiwanda sasa maana yangu ni nini? Maana yangu ni kwamba akinamama tunaviwanda lakini hatuvijui, kwa maana ya kuelewa neno kiwanda kila nyumba inayopika mboga na ugali ni kiwanda kwa sababu inabadilisha unga kuwa ugali”

“Kwa hiyo tunaposema kiwanda tusiwe tukafikiri ni jambo pana sana, ni jambo kubwa sana. akija mzungu hapa akapika maharage kwenye jiko, na akayaweka kwenye kopo tunasema hiki ni kiwanda lakini hakija huyu mama akipika maharage akayaweka kwenye sahani mkala hakiwi kiwanda. Kwa hiyo viwanda mnatembea navyo kazi ni kuviboresha tu, tuwe wabunifu viwe vizuri ili vipate soko.”

Awali akisoma risala kawa mgeni rasmi, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Ndg. Zena Kapama amesema kuwa, Halmashauri imeweka mkakati wa kutoa mikopo kutokana na pesa zamakusanyo ya ndani kila robo baada ya kutoa mara moja kwa mwaka kama iliyokuwa awali.

“Mhe. Mgeni rasmi katika kutekeleza azma ya Serikali ya kufikia maendeleo endelevu na malengo ya pamoja, pamoja na mkakati wa nchi yetu wa Serikali ya viwanda. Mkakati wetu Mhe. Mgeni rasmi ni kwamba kila robo tutakuwa tunatoa mikopo kwa kupitia fedha yetu ya makusanyo ya ndani kwa wanawake na vijana”

 

Matangazo

  • VITUO VYA KUJIANDIKISHIA ORODHA YA WAPIGA KURA October 11, 2024
  • TANGAZO LA KAZI YA KUJITOLEA KWA KAZI YA MSAIDIZI WA WATOTO MAHAKAMANI February 02, 2022
  • TANGAZO LA ZOEZI LA UTOAJI WA ANWANIZA MAKAZI March 04, 2022
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA March 16, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • KIAPO CHA UTII KWA WAUGUZI MBEYADC

    May 16, 2025
  • BI. ERICA AMEMTEMBELEA ASKALI ALIELAZWA HOSPITALI YA IFISI

    May 08, 2025
  • Mapokezi ya Mhe Mchengerwa MbeyaDc

    April 26, 2025
  • Karibu Mhe. Mchengerwa

    April 25, 2025
  • Tazama zote

Picha Mwendo

"Wapo Wakuu wa Idara na Vitengo wakiamishwa watu wanafanya sherere" Waitara Naibu waziri TAMISEMI
Picha mwendo zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MBEYA

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti ya mkoa wa Mbeya

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

writingMasterThesis

Mahali

Wasiliana nasi

    Mbaliz Road

    Sanduku la posta: 599

    Simu ya mezani: 025-2502260

    Simu ya mkononi: 0762210758

    Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera binafsi
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma zetu

Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.