Wauguzi Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya wamekula kiapo cha utii wa kuyaishi maisha ya kazi ya Uuguzi.
Kiapo hicho kimeongozwa na Muuguzi Mkuu wa Wilaya Bi Nitike Jackson Kyejo katika Viwanja vya Stendi ya Mbalizi (Tarafani) ikiwa ni siku ya Mwisho ya maadhimisho ya Wiki ya Wauguzi Duniani ambapo Kitaifa Siku ya Wauguzi iliadhimishwa mnamo tarehe 12 Mei, 2025 mkoani Iringa.
Sambamba na hilo Wauguzi hao wametoa huduma mbalimbali za Vipimo kwa wananchi bila malipo ikiwemo huduma ya Uzazi wa mpango, uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi Kwa wanawake, huduma ya macho, kupima presha (msukumo wa damu),kupima uzito,kupima hali ya maambukizi ya virusi vya ukimwi,kugawa kondom,Ushauri mbalimbali kuhusu Afya.
Halfa hiyo ya uapisho ilihudhuriwa na Mgeni rasmi Bi AgnessElikunda kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya (W) ya Mbeya Bi. Erica Yegella ambaye aliwashukuru Wauguzi kwa Utendaji kazi wao na kuwaahidi kuwa Serikali iko bega kwa bega na Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) katika kuhakikisha inatengeneza mazingira mazuri ya utendaji kazi na kulinda maslahi ya Wauguzi.
Mgeni rasmi alipata wasaa wa kutembelea mabanda yote na kushuhudia namna huduma za vipimo vya magonjwa mbalimbali zinavyotolewa.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.