Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Beatrice Urio, amewataka wananchi hususani vijana kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na Halmashauri ili kukuza mitaji yao na kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli wanazozifanya.
Bi. Beatrice Urio amesema hayo kwenye hafla ya utoaji tuzo za wajasiriamali zilizotolewa ndani ya ukumbi wa Tughimbe jijini Mbeya ambapo akimwakilisha Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya Erica E. Yegella.
Akizungumza na washiriki wa shughuli hiyo, Beatrice amesema mikopo inaendelea kutolewa katika Halmashauri zote nchini kutokana na mapato yake ya ndani hivyo ni fursa kwa wananchi kutumia fursa hiyo kukopa na kuendeleza shughuli wanazozifanya ikiwemo biashara na kilimo.
"Mikopo ipo na inaendelea kutolewa katika Halmashauri zote nchini na nyie mmeshaanza, kachukueni mikopo hiyo ili kuongeza uchumi wenu na biashara zenu kukua", amesema Bi Beatrice Urio.
Aidha amempongea Mkurugenzi aliyeanzisha tuzo hizo kwa lengo la kuwainua wajasiliamali na kwanba anaamini mwaka 2026 washiriki w
watakuwa wengi kuliko mwaka huu.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Ruvuma Women in Business (RWib) Bi Aneth Anania Nyanyinde amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji Bi Erica Yegella kwa kuitikia wito na kutuma mwakilishi ili kushirikiana nao kwenye tukio hilo la aina yake ikiwa limefanyika kwa mara ya kwanza Mbeya likijumuisha wajasiliamali kutoka maeneo ya mikoa ya Mbeya, Songwe na Songea mkoani Ruvuma.
Hafla hiyo ilikuwa na utoaji wa tuzo kwa wajasiliamalia na utoaji wa vyeti kwa wajasiliamali wapya.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.