Halmashauri ya wilaya ya Mbeya mkoani Mbeya imetoa na kukabidhi hundi ya mfano ya zaidi ya shilingi million mia saba kwa vikundi vya wajasiriamali, wakulima na maafisa usafirishaji 32 wilayani humo.
Mkopo huo umekabidhiwa na Mbunge wa Mbeya vijijini Mhe. Oran Njeza kwenye hafla iliyofanyika katika eneo la Tarafani mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi wilayani Mbeya.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Beatrice Ngutu akimwakilisha mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mbeya amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kwenda kuitumia vizuri kuinua uchumi wao, familia zao na Taifa kwa ujumla akisema mikopo hiyo sio zawadi.
Aron Sote ni afisa tarafa ya Isangati akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe. Solomon Itunda, amesema wako baadhi ya watu wakipata pesa huzitumia kwa mambo yasiyo ya msingi na lazima na kuwa watakaobainika kutumia mikopo hiyo vibaya watachukuliwa sheria.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mbeya vijijini Akimu Mwalupindi, ameipongeza Halmashauri ya Mbeya kwa kuhakikisha mikopo hiyo inatolewa.
Kwa mujibu wa ofisi ya maendeleo ya jamii Halmashauri ya wilaya ya Mbeya chini ya bi. Agness Elkunda, jumla ya vikundi 32 vinavyojihusisha na shughuli mbalimbali vimepata mikopo hiyo kwa kipindi cha robo mwaka pekee na kwa miaka mitano zaidi ya shilingi Billion nne na nusu zimetolewa na kukopeshwa kwa wananchi mbalimbali bila riba yoyote na kuomba uaminifu kwa wakopaji na kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili kuwanufaisha wananchi wengine.
Mgeni rasmi Mhe. Mbunge wa Mbeya vijijini Oran Manase Njeza, amesema mikopo hiyo ni takwa la kikanuni ambalo Serikali ilishajiwekea kurejesha fedha hizo kwa wananchi kwa njia ya mikopo ya bila riba na kwamba CCM iliahidi kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.