Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imewaagiza walimu wa Hesabu kuacha tabia ya kutumia namba zao za siri katika steshenari za kompyuta (stationary), kwani haitoi usalama wa kutosha na inaweza kusababisha wizi wa taarifa bila wao kufahamu.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Bi. Yegella, wakati akifungua mafunzo ya siku moja kuhusu matumizi ya mfumo wa FFAIRS kwa walimu wa hesabu.
Akizungumza na walimu hao, Bi. Yegella amesema kuwa tabia ya kuandika au kutoa namba za siri ndani ya steshenari ni hatari na sio salama.
“Walimu wengi wanatoa namba zao za siri katika steshenari, jambo ambalo si zuri na linaweza kusababisha wizi bila wao kufahamu,” alisema Bi. Yegella.

Bi. Yegella amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea walimu uelewa sahihi wa kutumia mifumo ya kidigitali kwa njia salama, hasa wakati wa kuingiza taarifa za hesabu na takwimu za shule kwenye mfumo wa FFAIRS.
Aidha, amewataka walimu kukumbatia taratibu za usalama wa taarifa ili kulinda data za shule na wanafunzi dhidi ya matumizi mabaya au upotevu wa taarifa muhimu.
Mafunzo ya siku moja yanahusisha maelekezo ya kinaga ubaga juu ya namna ya kuingia na kutumia mfumo wa FFAIRS kwa ufanisi bila kuathiri usalama wa taarifa. Walimu waliohudhuria mafunzo hayo wameonyesha kuridhika na maarifa mapya waliyopata, na kusema yatasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao ya kazi.

Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.