• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za watumishi |
Mbeya District Council
Mbeya District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya Mbeya

  • Nyumbani
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mifugo na uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA na Mahusiano
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi
      • Ufugaji wa nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Wataalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
      • Taarifa ya fedha
      • Mpango wa Mapato na Matumizi
      • Mapato na Matumizi ya Mwezi
      • Taarifa ya miradi ya maendeleo
      • Taarifa ya fedha ya mwaka
      • Mihtasari ya Mikutano ya Baraza
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
      • Mwongozo wa Matumizi ya Vifaa vya TEHAMA
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Picha mwendo
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Mradi wa Maji Izumbwe, Iwindi, Mwashiwawala kukamilika mwezi Juni, 2018

Imewekwa: April 2nd, 2018

Mradi wa maji wa Izumbwe, Iwindi, Mwashiwawala unatarajiwa kukamilika mwezi juni, 2018. Kukamilika kwa mradi huu wananchi zaidi ya elfu 14 wa vijiji vya izumbwe, Iwindi na Mwashiwawala watanufaika kwa kupata maji safi na salama.

Mhandisi wa Maji, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Vivian Mndolwa amesema mradi huu ulianza kujengwa mwezi  Machi, 2017 na ulitarajiwa kukamilika mwezi Disemba 2017. Lakini kutokona na mvua kubwa zilizonyesha zimesababisha mradi kusimama kwa muda hivyo utamalizika mwezi Juni, 2018.

“Mradi huu ulianza kutekelezwa machi 2017 na mkataba wa mradi huu ni wa miezi 9. Na tulitegemea tungemaliza mwezi wa 12 lakini kwa sasa tutamaliza mwezi Juni 2018… kwa sababu mamboa yote yapo, isipokuwa kilichokuwa kinazuia ni hizi mvua zinazonyesha wangechimbwa mitalo ingekuwa inajifukia”

Gharama za mradi huu ni Shilingi bilioni 1.5 ambapo mpaka sasa pesa zilizotumika ni Shilingi Milioni 562,122,764/- Kazi zilizofanyika ni ujenzi wa matanki yote matatu yenye ukubwa wa lita 45,000, 90,000 na135,000. Ujenzi wa vituo 38 vya kuchotea na ununuaji wa mabomba ya usambazaji maji yenye urefu wa mita 61,213. Kazi zilizobaki ambazo hadi kufikia Juni, 2018 zitakuwa zimekamilika ni ujenzi wa vituo vingine 38 vya kuchotea maji pamoja na ulazaji wa mabomba.

Diwani wa Kata ya Igale, Mhe. Maiko Mwasonzwe ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa kutekeleza mradi huu ambao ni muhimu kwa wananchi wakata yake pamoja na kata jirani ya iwindi. Mhe. Mwasonzwe amesema mradi huu utakakapo kamilika utakuwa ni suluhisho la kudumu la tatizo la maji katika eneo lake kwani wananchi wamekuwa wakipata hadha kubwa ya ukosefu wa maji.

“Wananchi wameusubiri mradi huu kwa muda mrefu na wanapata shida ya kutafuta maji naamini kwamba mradi ukikamilika itakuwa ni mkombozi kwa wanachi wangu wa kata ya igale na kata ya Iwindi ambao wanategemea mradi huu wa maji”

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Izumbwe ambao nao ni wanufaika wa mradi huu pindi utakapokamilika wamesema kuwa tatizo la maji tatizo la maji katika kijiji chao linaenda kuwa historia. Hivyo wamesemapindi mradi huo utakapo kamilika kufika mwezi Juni wataupokea kwa furaha, lakini kubwa zaidi watautunza mradi huo kama  wanavyotunza miradi mingine inayotekelezwa na Serikali katika kijiji chao. Dick Paulenje mkazi wa kijiji hicho amesema

“Huu mradi ukikamilika kufikia mwezi wa sita tutaupokea vizuri sana kuufurahia kwa sababu tutakuwa tunanufaika na uhitaji wa maji yenyewe maana maji yanauhitaji mwingi tu, kuna kumwagilia, kupikia na mengine mengi tu ya kibinadamu, nadhani yatakuwa yametusaidia sana na niahidi sisi kama wananchi tutautunza mradi huu illi kulifanya tatizo la maji kuwa historia katika kijiji chetu”

Matangazo

  • VITUO VYA KUJIANDIKISHIA ORODHA YA WAPIGA KURA October 11, 2024
  • TANGAZO LA KAZI YA KUJITOLEA KWA KAZI YA MSAIDIZI WA WATOTO MAHAKAMANI February 02, 2022
  • TANGAZO LA ZOEZI LA UTOAJI WA ANWANIZA MAKAZI March 04, 2022
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA March 16, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • KIAPO CHA UTII KWA WAUGUZI MBEYADC

    May 16, 2025
  • BI. ERICA AMEMTEMBELEA ASKALI ALIELAZWA HOSPITALI YA IFISI

    May 08, 2025
  • Mapokezi ya Mhe Mchengerwa MbeyaDc

    April 26, 2025
  • Karibu Mhe. Mchengerwa

    April 25, 2025
  • Tazama zote

Picha Mwendo

"Wapo Wakuu wa Idara na Vitengo wakiamishwa watu wanafanya sherere" Waitara Naibu waziri TAMISEMI
Picha mwendo zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MBEYA

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti ya mkoa wa Mbeya

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

writingMasterThesis

Mahali

Wasiliana nasi

    Mbaliz Road

    Sanduku la posta: 599

    Simu ya mezani: 025-2502260

    Simu ya mkononi: 0762210758

    Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera binafsi
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma zetu

Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.