Katibu Mkuu Wizara ya Habari Michezo na Utamaduni ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Bwana Gerson Msigwa amepongeza na kufurahishwa na kazi nzuri ya Maafisa Habari ngazi ya Mikoa na Halmashauri nchini katika kutangazana kueneza mafanikio mbalimbali ya serikali kwa wananchi wake.
Pongezi hizi amezitoa wakati akifunga kikao kazi cha Maafisa Habari kilichoketi kwa muda wa siku mbili kuanzia jana tarehe 23.5.2025.
Msigwa amesema Serikali imetekeleza Miradi mbalimbali katika ngazi ya Halmashauri hatua ambayo imesaidia wananchi kupata huduma karibu na makazi yao hivyo maafisa Habari hawana budi kuhakikisha wanaitolea kwa taarifa kwa Wananchi na thamani ya fedha iliyotolewa.
"Serikali imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya afya, elimu, maji, umeme na barabara hivyo ni jukumu la afisa habari kuitangaza miradi hii kwa ufanisi mkubwa"
Aidha amewakumbusha Maafisa Habari kuendelea kushirikiana na Vyombo vingine vya habari ikiwemo, redio , Magazeti, Mitandao ya Kijamii na Televisheni katika kufikisha maadhui ya serikali kwa Wananchi wake.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.