• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za watumishi |
Mbeya District Council
Mbeya District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya Mbeya

  • Nyumbani
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mifugo na uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA na Mahusiano
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi
      • Ufugaji wa nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Wataalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
      • Taarifa ya fedha
      • Mpango wa Mapato na Matumizi
      • Mapato na Matumizi ya Mwezi
      • Taarifa ya miradi ya maendeleo
      • Taarifa ya fedha ya mwaka
      • Mihtasari ya Mikutano ya Baraza
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
      • Mwongozo wa Matumizi ya Vifaa vya TEHAMA
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Picha mwendo
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

REA KUSAMBAZA UMEME VITONGOJI 114 MBEYA DC MAPEMA MWAKA HUU

Imewekwa: February 13th, 2026

Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya (Mbeya DC) inatarajia kuanza utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) katika vitongoji 114.

Mradi huo unakadiriwa kugharimu shilingi bilioni 3.6, ukilenga kuwawezesha wananchi kupata nishati ya umeme kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi na kuchochea maendeleo ya kijamii.

Taarifa hiyo imetolewa na Msimamizi wa Miradi ya REA kutoka Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) Wilaya ya Mbeya, wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mbeya DC kilichoketi kujadili na kupitisha Rasimu ya Mapendekezo ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027.

Akizungumza katika kikao hicho, Msimamizi huyo alisema kuwa maandalizi ya awali ya utekelezaji wa miradi hiyo tayari yamekamilika.

“Mikataba ya miradi hii tayari imesainiwa, na mkandarasi wa kusimamia utekelezaji ameshapatikana. Aidha, mkandarasi huyo tayari ameanza kazi katika maeneo yanayopakana na Mbeya DC. Hivyo, tunapaswa kujiandaa mapema kwani kabla ya mwezi huu Februari 2026 kuisha tutaanza rasmi utekelezaji wa miradi katika vitongoji vyote 114 vilivyopo kwenye mpango wa umeme kulingana na bajeti,” alisema.

Kwa upande wake, Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Wilaya ya Mbeya, Christina Shoki, amewatahadharisha wananchi kuwa makini katika maeneo ambayo miundombinu ya umeme itapita wakati wa utekelezaji wa mradi, ili kuepusha ajali na madhara yanayoweza kujitokeza.

Ameeleza kuwa bado kuna baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema wanaojihusisha na hujuma za miundombinu ya umeme, ikiwemo wizi wa mafuta ya transfoma na nyaya za shaba (copper), hali inayohatarisha maisha yao na kuisababishia hasara TANESCO.

“Tabia hii iliwahi kukoma, lakini kwa sasa imeanza kujitokeza tena. Watu wameanza kuiba mafuta ya transfoma pamoja na nyaya za shaba. Vifaa hivi vina umuhimu mkubwa katika uendeshaji wa transfoma. Vinapoibiwa, husababisha mashine kuungua na shirika hulazimika kununua transfoma mpya kwa gharama kubwa. Madiwani mtusaidie kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo yenu kuhusu athari za vitendo hivi." alisisitiza Shoki.

Matangazo

  • VITUO VYA KUJIANDIKISHIA ORODHA YA WAPIGA KURA October 11, 2024
  • TANGAZO LA KAZI YA KUJITOLEA KWA KAZI YA MSAIDIZI WA WATOTO MAHAKAMANI February 02, 2022
  • TANGAZO LA ZOEZI LA UTOAJI WA ANWANIZA MAKAZI March 04, 2022
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA March 16, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • REA KUSAMBAZA UMEME VITONGOJI 114 MBEYA DC MAPEMA MWAKA HUU

    February 13, 2026
  • MBEYA DC YASAJILI 483 BIMA YA AFYA KWA WOTE

    February 13, 2026
  • MWENYEKITI MBEYA DC AKABIDHI VISHIKWAMBI 44 KWA MADIWANI KUIMARISHA UFANISI WA KAZI

    February 13, 2026
  • MKURUGENZI, WATENDAJI VIJIJI MBEYA DC WAJADILI MIKAKATI KUHARAKISHA MAENDELEO

    February 12, 2026
  • Tazama zote

Picha Mwendo

"Wapo Wakuu wa Idara na Vitengo wakiamishwa watu wanafanya sherere" Waitara Naibu waziri TAMISEMI
Picha mwendo zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MBEYA

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti ya mkoa wa Mbeya

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

writingMasterThesis

Mahali

Wasiliana nasi

    Mbaliz Road

    Sanduku la posta: 599

    Simu ya mezani: 025-2502260

    Simu ya mkononi: 0762210758

    Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera binafsi
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma zetu

Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.