• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za watumishi |
Mbeya District Council
Mbeya District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya Mbeya

  • Nyumbani
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mifugo na uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA na Mahusiano
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi
      • Ufugaji wa nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Wataalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
      • Taarifa ya fedha
      • Mpango wa Mapato na Matumizi
      • Mapato na Matumizi ya Mwezi
      • Taarifa ya miradi ya maendeleo
      • Taarifa ya fedha ya mwaka
      • Mihtasari ya Mikutano ya Baraza
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo
      • Mwongozo wa Matumizi ya Vifaa vya TEHAMA
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Picha mwendo
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Waheshimiwa Madiwani wakumbushwa kutekeleza ahadi zao

Imewekwa: May 23rd, 2017

Waheshimiwa Madiwani wakumbushwa kutekeleza ahadi zao

Takribani miezi 19 sasa imepita sawa na mwaka mmoja na miezi saba tangu uchaguzi mkuu ufanyike tarehe 25 Oktoba 2017. Uchaguzi Mkuu nchini hufanyika kila baada ya miaka mitano ambapo raia wa Tanzania wenye umri kuanzia miaka 18 hupata fursa ya kuwachagua wawakilishi wao; yaani waheshimiwa madiwani, wabunge pamoja na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

 Katika uchaguzi wa 25Oktoba 2017 wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya nao walipata fursa hiyo ya kuwachagua wawakilishi wao ambapo kwa ngazi ya kata waliweza kuwachagua waheshimiwa madiwani 38, kati ya hao 28 waliogombea kwenye kata na 10 walipita kwa nafasi ya Udiwani  Viti Maaluma.

Bila chembe ya shaka yoyote wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya waliwachagua viongozi hao baada ya kuridhishwa na ahadi walizozitoa wakati wa kampeni iliyofanyika kwa miezi mitatu kabla ya tarehe ya uchaguzi. Bw. Costantino Mushi Afisa Serikali za Mitaa toka Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya amewakumbusha Waheshimiwa madiwani kutekeleza ahadi zao walizoziahidi wakati wa kampeni ili kuwajengea imani wananchi na serikali waliyoichagua.

Bw. Mushi ameyasema hayo kwenye Mkutano wa baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya alipomwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Bi. Rehema Mtunguja. Bw. Mushi amesema ahadi nyingi walizozitoa madiwani zinalenga kuwapelekea maendeleo wananchi katika maeneo yao, hivyo wakati muafaka wa kutekeleza ahadi hizo ni sasa kabla ya kusubiri uchaguzi mwingine utakaofanyika mwaka 2020.

Bw. Mushi amesema ili kutekeleza ahadi hizo kwa urahisi ni vyema waheshimiwa madiwani wakaweka maslahi ya wananchi mbele badala ya kuangalia maslahi yao binafsi.  Pia amesema ni vyema madiwani wakaongeza nguvu katika kukusanya mapato ili fedha zitakazo patikana zipelekwe kutekeleza ahadi hizo.

“Tuweke maslahi ya wananchi mbele badala ya maslahi yetu sisi binafsi, tufanye kazi kwa kumuangalia mwananchi wa kawaida ambaye ametuleta katika baraza hili. Na niseme kwamba kunaahadi nyingi mmeahidi kule kwa wananchi, siku zinayoyoma, mapato pengine hayakidhi, miradi haitekelezeki sasa mtapoteza muda na watu ambao hawaisaidii tena hii Halmashauri badala ya kukazana kukusanya mapato zaidi na kuelekeza kule kwa wananchi ili zile ahadi ulizoahidi wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Taifa wa mwaka 2015 ziweze kutekelezeka”

Pia Bw. Mushi amesema ili Halmashauri hii iweze kufikia lengo katika kukusanya mapato  ni vyema waheshimiwa madiwani wakashirikiana wataalamu.

“Napenda kusisitiza katika kukusanya mapato, wiki iliyopita nimeona mmefikia zaidi ya asilimia 60 la lengo lenu la mwaka. Lakini muda umekwisha na tumeagizwa kufikia asilimia 100 ikifika tarehe 30 Juni. Kama hamkufikia asilimia 100 ni lazima muweke sababu za msingi kwanini hamkufikia lengo. Kwa hiyo kwa hili ninaomba mshirikiane na watendaji wala msiwaachie wao wenyewe”

Matangazo

  • VITUO VYA KUJIANDIKISHIA ORODHA YA WAPIGA KURA October 11, 2024
  • TANGAZO LA KAZI YA KUJITOLEA KWA KAZI YA MSAIDIZI WA WATOTO MAHAKAMANI February 02, 2022
  • TANGAZO LA ZOEZI LA UTOAJI WA ANWANIZA MAKAZI March 04, 2022
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA March 16, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • KIAPO CHA UTII KWA WAUGUZI MBEYADC

    May 16, 2025
  • BI. ERICA AMEMTEMBELEA ASKALI ALIELAZWA HOSPITALI YA IFISI

    May 08, 2025
  • Mapokezi ya Mhe Mchengerwa MbeyaDc

    April 26, 2025
  • Karibu Mhe. Mchengerwa

    April 25, 2025
  • Tazama zote

Picha Mwendo

"Wapo Wakuu wa Idara na Vitengo wakiamishwa watu wanafanya sherere" Waitara Naibu waziri TAMISEMI
Picha mwendo zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MBEYA

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti ya mkoa wa Mbeya

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

writingMasterThesis

Mahali

Wasiliana nasi

    Mbaliz Road

    Sanduku la posta: 599

    Simu ya mezani: 025-2502260

    Simu ya mkononi: 0762210758

    Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera binafsi
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma zetu

Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.