Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya leo Februari 17, 2026 wamepatiwa mafunzo maalum kuhusu afya ya akili na magonjwa yasiyoambukiza katika ukumbi wa Halmashauri.
Mafunzo hayo yametolewa na Dkt. Garvin Kweka kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, yakilenga kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kutunza afya ya akili, kutambua dalili za awali za changamoto za kisaikolojia pamoja na mbinu za kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, shinikizo la damu, saratani na magonjwa ya moyo.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Dkt. Kweka alisisitiza kuwa afya ya akili ni sehemu muhimu ya ustawi wa mtumishi na ina mchango mkubwa katika kuongeza ufanisi kazini. Aidha, aliwahimiza watumishi kuzingatia mtindo bora wa maisha unaojumuisha lishe sahihi, mazoezi ya mara kwa mara, kupunguza msongo wa mawazo na kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara.
Mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za halmashauri katika kuboresha ustawi wa watumishi wake na kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.