Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Cuthbert Mwinuka, amezitataka kampuni zinazojihusisha na zao la pareto kuzalisha mbegu bora na kuzisambaza kwa wakulima ili kuongeza ubora na tija ya pareto inayozalishwa Mbeya.
Mwinuka alitoa wito huo wakati wa kikao chake na kampuni tisa (9) zinazonunua zao la pareto kutoka kwa wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya. Alisema kuwa uzalishaji wa mbegu bora utasaidia kuinua kiwango cha uzalishaji, kuboresha ubora wa mazao na kuongeza kipato kwa wakulima.
“Ni muhimu kampuni hizi zikishiriki kikamilifu katika mnyororo wa thamani kwa kuzalisha mbegu bora na kuwafikishia wakulima kwa wakati. Hii itasaidia kupata pareto yenye ubora zaidi na yenye ushindani kwenye soko,” alisema Mwinuka.

Mbali na hilo, aliwataka wawakilishi wa kampuni hizo kuhakikisha wanalipia ushuru wa zao ili wapate vibali vya usafirishaji na kuondoa usumbufu usio wa lazima katika shughuli za ununuzi wa zao hilo.
Aidha, Mwinuka alisisitiza umuhimu wa kutoa elimu kwa wakulima kuhusu njia bora za utunzaji wa zao la pareto kuanzia vitaluni, shambani hadi wakati wa mavuno na ukaushaji akieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kudumisha ubora wa zao hilo na kuongeza thamani yake soksokon.
Kampuni zilizoshiriki kikao hicho ni Paytech, PCLT, Anda Ltd na mengine sita yanayojihusisha na ununuzi na usindikaji wa pareto katika Wilaya ya Mbeya.
Hatua hiyo inatarajiwa kuimarisha sekta ya pareto na kuongeza mchango wake katika uchumi wa wakulima pamoja na taifa kwa ujumla.

Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.