Ardhi bora inayofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali mfano Mahindi,Maharage, Viazi mviringo /Vitamu,Ngano,Kahawa, Pareto, Alizeti,Ufuta na Mazao ya bustani yote.
Hali ya hewa inayofaa kwa kilimo kwa mwaka mzima wa uzalishaji wa mazao.
Miundo Mbinu ya Umwagiliaji iliyoboreshwa yenye uwezo wa kumwagilia jumla ya hekta 2450.
Wataalamu wa kilimo wa kutosha kuhudumia wakulima kwa kipindi chote cha uzalishaji wa mazao
Miundo Mbinu bora ya usafirishaji toka mashambani hadi kwenye Masoko ya mazao
Maghala ya kuhifadhi mazao ya nafaka na mikunde kwa mwaka mzima wa kilimo.
Upatikanaji rahisi wa Pembejeo za kilimo toka makampuni mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
Masoko ya mazao ya kilimo yanapatikana kwa urahisi toka ndani na nje ya nchi (Malawi, Zambia,DRC-Congo,Burundi na Rwanda).
Upatikanaji rahisi wa nguvu kazi katika Wilaya yenye zaidi ya wakazi 305,319 .