Mkoa wa Mbeya kupitia Halmashauri zake imetoa taarifa ya mwenendo wa uandikishaji wapiga kura wa uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika kuanzia Tarehe 11 hadi 20/10/2024 ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imekuwa ya pili kwa asilimia 97.7, amesema Msimamizi Mkuu wa uchaguzi Ndug. Gidion Mapunda.
Kwamujibu wa makadirio ya wapiga kura Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kupitia takwimu za NBS-2024 zinaonyesha Wanaume 93,145 na Wanawakeni 116,038 waliojitokeza kujiandikisha kupiga kura hivyo jumla ya waandikishaji ni 209,183.
Aidha uandikishaji halisi wa kila siku kwa tarehe 11 -20/10/2024 waliojitokeza wanaume ni 94,694 na wanawake ni 109,631 jumla yao ni 204,325.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.