TEHAMA
KITENGO CHA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO(TEHAMA)
Kitengo Cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kina jukumu la kutoa huduma za kitaalamu juu ya matumizi ya Teknolojia ya habari na mawasiliano kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Majukumu ya Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
Kutayarisha Mpango Mkakati wa kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Miongozo na taratibu kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya TEHAMA.
Kuishauri Menejimenti ya Halmashauri juu ya masuala yanayohusiana na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na utekelezaji wa dhana ya serikali mtandao.
Kusimamia maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na utekelezaji wake kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya.
Kushirikiana na OWM-TAMISEMI kuratibu na kuendeleza viwango vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa ajili ya “software na hardware” kwa matumizi ya Halmashauri na Mamlaka ya Mji mdogo.
Kuiwezesha Mamlaka ya Mji Mdogo, Kata na vijiji katika kuendeleza na kutekeleza mipango/miradi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Kuratibu utekelezaji,usanifu,utunzaji na uendelezaji wa matumizi ya Tovuti na utunzaji wa kumbukumbu kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya, Wizarai na wadau wengine.
Kutathimini, kuboresha na kusimamia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na usimamizi wa mifumo ya taarifa/habari iliyosimikwa/iliyowekwa kwenye Halmashauri.
Kufanya tathimini ya mahitaji ya mafunzo juu ya usimamizi wa mifumo ya taarifa na teknolojia ya habari na mawasiliano na kuandaa mpango wa kujenga uwezo kwa watumishi wa Kitengo cha TEHAMA na watumiaji wengine wa mifumo.
Kufanya tathimini ya hatari/hasara zinazohusiana na miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na mfumo wa usimamizi wa taarifa na namna ya kuthibiti.
Kuendeleza na kutunza Tovuti ya Halmashauri.
Kuratibu masuala yakiitifaki ikiwemo kupokea wageni.
Usimamizi wa mifumo ya kompyuta(SystemAdministration)
Usimamizi wa mtandao wa kompyuta pamoja na vifaa vyake (Network And HardwareAdminstration).
Usimamizi wa benki ya takwimu(Database Administration)
Usimamizi wa tovuti na barua pepe (website administration & emails).
Kutekeleza na kusimamia sera ya TEHAMA na Serikali Mtandao.
Kuandaa mahitaji katika Ununuziwa vifaa vya TEHAMA.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.