Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya inaongozwa na Baraza la Madiwani ambacho ndicho chombo kikuu cha maamuzi. Kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya za Mwaka 2013 kanuni ya 40 (1) Halmashauri kupitia mkutano wa mwaka itateua wajumbe wa kamati mbalimbali za kudumu, ikiwema kamati ya Elimu, Afya na Maji.
Mbali na majukumu mengine, jukumu mahususi la Kamati hii ni kushughulikia mambo yote yanayohusu afya ya jamii, elimu na huduma za maji,ikiwa ni pamoja na kuangalia jitihada za wanannchi vijijini kujiletea maendeleo yao kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushauri, kushawishi, kuzindua, kuelimisha na kushirikisha wananchi hao hasa katika kutayarisha, kutekeleza, kusimamia na kutathmini mipango yao ya maendeleo.
WAJUMBE WA KAMATI YA ELIMU, AFYA NA MAJI
Kama ilivyoelezwa hapo juu kuwa kupitia Mkutano wa Mwaka Baraza la Madiwani linajukumu kubwa ya kufanya uteuzi wa wajumbe wa kamati mbalimbali za kudumu ikiwemo kamati ya Elimu, Afya na Maji.
Ifuatayo ni orodha ya wajumbe wa kamati ya Elimu, Afya na Maji kwa mwaka 2017/2018
Orodha ya wajumbe wa kamati ya Elimu, Afya na Maji.pdf
MAJUKUMU YA KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO.
Kamati ya Elimu, Afya na Maji inatekeleza majuku yake kisheria kama yalivyoainishwa kwenye Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya za Mwaka 2013. Majukumu hayo ni kama ifuatavyo:
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.