HALMASHAURI YA WILAYA YA MBEYA
1.1 HISTORIA YA HALMASHAURI
Halmashauri ya wilaya ilianzishwa mwaka 1984 kama Halmashauri ya wilaya baada ya kuanza kufanya kazi Sheria ya Serikali za Mitaa(Mamlaka za Wilaya) Na. 7(1982). Chini ya mkurugenzi John T. Matata 1984-1990, Orodha ya wakurugenzi waliopita katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya ni pamoja na John T. Matata, Daudi J. Mwabulambo 1990- 1996, Joseph J. Kahale 1996- 1996, Solanus M. Nyimbi 1996- 2005, Raphael . k. Kimoleta, 2005-2006, Juliana T. Malance 2006-2012, Upendo A. Sanga 2012- 2016, Amelchiory M. Kulwizila 2016 – 2018 pamoja na Stephe E. Katemba 2018 hadi sasa.
1.2 MIPAKA NA UTAWALA
Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ni moja kati ya Halmashauri saba (7) za Mkoa wa Mbeya; zingine ni Mbarali, Chunya, Kyela, Rungwe, Busokelo na Jiji la Mbeya. Halmashauri hii iko kati ya Latitude 7° na 9° Kusini mwa Ikweta na Longitude 33° na 35° Mashariki mwa Greenwich. Wilaya inapakana na Wilaya ya Mbarali na Makete kwa upande wa Mashariki, Rungwe na Ileje upande wa kusini, Magharibi imepakana na Mbozi, Momba na Kaskazini Wilaya ya Chunya.
Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya inaundwa na Tarafa tatu ambazo ni Tembela, Isangati na Usongwe. Baada ya kuanzishwa kwa Mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi mwaka 2014, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya inajumla ya Kata ishirini na nane (28), Vijiji 140 na Vitongoji 931 vyenye jumla ya kaya 74,468.
Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ina jumla ya Madiwani 38, kati ya hao 28 ni madiwani wa kuchaguliwa na 10 ni Madiwani wa viti maalum. Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya inajimbo moja la ubunge linalojulikana kama jimbo la Mbeya vijijini. Pamoja na Baraza la Madiwani maamuzi ya Halmashauri yanafikiwa kwa kupitia Kamati zake za kudumu nne (4) ambazo ni:
(i) Fedha, Uongozi na Mipango
(ii) Elimu, Afya na Maji
Uchumi, Ujenzi na Mazingira
UKIMWI
ENEO LA ARDHI.
Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ina eneo la Ukubwa wa Kilometa za Mraba 2,432 ambazo ni sawa na hekta 243,200. Eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 216,400 sawa na asilimia 88.9.
IDADI YA WATU
Kwa mujibu wa matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Halmashauri ina jumla ya wakazi 305,319 kati yao wanaume ni 143,779 na wanawake ni 161,540 sawa na ongezeko la asilimia 2.5 kwa mwaka. Msongamano wa watu kwa eneo ni watu 127.6 kwa kilometa ya mraba (km²).
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.