1.0 UTANGULIZI
Kitengo hiki ni kimoja kati ya vitengo 6 katika Halmashauri ya Mbeya. kitengo hiki ni kiungo maalum kinacho ratibu shughuli zote za uchaguzi wa Uchaguzi Mkuu, serikali za za Mita na uchaguzi mdogo katika Halmashauri.
MAANA YA CHAGUZI MKUU
Uchaguzi ni njia ya msingi iliyokubalika ambayo jamii huitumia kupata viongozi Kidemokrasia. Sifa mojawapo ya Uchaguzi wa Kidemokrasia uliohuru na wa haki ni Uchaguzi kufanyika kwa Siri ambapo jamii hupiga Kura kwa viongozi wanao wahitaji na wanaowaona wanafaa kwa ajili ya kuwaongoza
Uchaguzi wa Kidemokrasia hufanyika mara kwa mara katika vipindi vinavyoeleweka, Uchaguzi kutoa fursa sawa kwa wagombea wote katika ngazi husika kuruhusu waangalizi wandani na nje kufuatilia mchakato mzima wa Uchaguzi.
Uchaguzi Mkuu
Ni mchakato mzima wa wananchi au jamii kupiga Kura kuchagua wawakilishi wao kuanzia ngazi ya kata kwa maana ya Madiwani, Jimbo kwa maana ya Wabunge na Uchaguzi wa Rais wa nchi.
Uchaguzi Mdogo
Ni Uchaguzi unaofanywa angalau mara mbili kwa Mwaka ili kuwapata Viongozi wa kujaza nafasi zilizo wazi katika Kata au Majimbo kutokana na sababu mbalimbali. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 13 (1) na (3) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292 na kifungu cha 37 (1) (b) na (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na;
Aidha Uchaguzi Mdogo huratibiwa na kusimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada ya kupokea taarifa ya maandishi kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kuhusu uwepo wa nafasi wazi za Udiwani.
Kila baada ya Uchaguzi Mkuu, Madiwani waliochaguliwa huchaguana na kuwapata Mwenyekiti na Makamu wa Halmashauri ya Wilaya ambao huungana na Mkurugenzi kama Katibu kuendesha shuguli za Halmashauri.
Halikadhalika madiwani waliochaguliwa pamoja na Mbunge wa Jimbo huunda kamati 5 ambazo hurahisisha utekelezaji na ufuatiliaji wa majukumu yao. Kamati ambazo huundwa ni
Jimbo la uchaguzi
Jimbo la uchaguzi la Mbeya vijijini lina Tarafa 3, kata 28, Vijiji 152 na Vitongoji 935 ambavyo hivi ni vituo vya kupigia kura na vituo 302 vya kuandikisha wapiga kura.
Halikadhalika jimbo lina Mbunge moja ambalo kwa sasa linaongozwa na Mhe. ORAN NJEZA wa kuchaguliwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyeibuka mshindi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Aidha Madiwani Ishirini na nane (28) waliibuka washindi katika uchaaguzi Mkuu huo, kati yao Madiwani ishirini na moja (21), wa Chama Cha Mapinduzi na saba ni wa (7) CHADEMA. Halikadhalika kuna Madiwani wawakilishi wa viti maalum, CCM wapo saba (7) na CHADEMA ni watatu (3), hivyo Jumla ya Madiwani wote wa Halmashauri kuwa Thelathini na nane (38)
Hali ya kisiasa katika Halmashauri ni shwari na wananchi wanaedelea na shughuli za maendeleo na zile za kujiongezea kipato. Kuna jumla vyama vya siasa kumi na moja (11) vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu wa 2015, vyama hivi ni kama vifuatavyo.
2.0 MAJUKUMU YA IDARA
Kitengo hiki kinasimamia Chaguzi zote za Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu
Kutambua nafasi wazi za viongozi wa kuchaguliwa ngazi za vijiji na vitongoji na kuhakikisha kuwa zinajazwa kwa wakati kwa kusimamia na kufanya uchaguzi mdogo katika vijiji/Vitongoji vilivyobainika kuwa havina viongozi wa kuchaguliwa mara tu nafasi inapotokea.
Kutoa taarifa ya utekelezaji pamoja na matokeo ya Viongozi waliochaguliwa ili kuwepo na kumbukumbu sahihi za ofisi
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.