MAJUKUMU YA SEKTA YA USAFI NA MAZINGIRA:
Kuboresha hali ya usafi wa mazingira ya jiji la Tanga kwa kufanya yafuatayo:
Kimarisha huduma za udhibiti wa taka ngumu, usafi wa barabara, maeneo na mifereji ya maji ya mvua.
Kuratibu utoaji huduma za maji taka na kuimarisha usafi wa mazingira.
Kusimamia huduma ya udhibiti wa hifadhi na usalama wa mazingira.
Kuimarisha programu ya elimu jamii kuhusu usafi wa mazingira, uchangiaji ada za udhibiti taka na uzingatiaji wa sheria.
Kuimarisha ukaguzi, usimamizi na ufuatiliaji wa usafi wa majengo na siha ya mazingira na afya ya jamii
Kuimarisha ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa ya milipuko
Kuimarisha huduma za udhibiti wa usalama na ubora wa chakula na vipodozi
Kuimarisha huduma za udhibiti ubora na usalama wa maji na usafi wa mtu binafsi (Hygiene)
MFUMO WA UDHIBITI WA UCHAFUZI WA MAZINGIRA.
TARATIBU ZA UTOAJI ADHABU KWA WACHAFUZI WA MAZINGIRA
Baada ya kukamatwa kwa wale wanaokaidi sheria na taratibu za usafi, watatozwa faini ya papo kwa hapo kwa makosa yanayostahili. Faini hiyo itatozwa na Afisa Mtendaji wa Kata na ama Afisa mwingine yeyote aliye chini yake na ambaye amemwidhinisha kwa barua kufanya kazi hiyo.Kwa makosa yasiyostahili faini ya papo kwa hapo, watuhumiwa watafikishwa katika mabaraza ya usuruhishi ya kata ama mahakamani.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.