Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe Beno Malisa ameongea na kamati ya Afya ya Wilaya kwenye kikao cha kamati ya afya ya msingi ya wilaya Kwa ajili ya maandalizi ya kampeni ya chanjo ya surua rubela kilicho keti leo tarehe 09.02.2024 katika ukumbi wa Meya Jijini Mbeya.
Mhe Malisa ameiambia kamati hiyo kwenda kuelimisha wananchi ili waweze kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wahudumu watakao kuwa wanapita kuwapatia chanjo hiyo watoto.
Hamasa zinaendelea ambapo waratibu wa afya watatoa elimu katika vyombo vya habari.
Chanjo ya Surua Rubela inaanza kutolewa kuanzia tarehe 15-18 itakayodumu kwa muda wa siku nne na inatolewa kwa watt kuanzia miezi 9 hadi miaka minne na miezi 11.
Chanjo hii inatolewa kwenye vituo vya kutolea huduma, kanisani,msikitini,hospitalini na sehemu zote wanaopatikana watoto.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.