SHULE YA SEKONDARI YA LWANJILO KUANZA 2024
Wanakijiji wa Lwanjilo wamemshukuru Rais Dkt Samia kwa kuwaletea shule ya sekondari kijijini kwao, shule ya sekondari Lwanjilo ndo shule ya kwanza kujengwa kijijini hapo, kijijini hapo kuna shule moja ya awali na msingi.
Lwanjilo Secondari ni moja ya shule zinazojengwa kwa fedha zilizoletwa na Rais Dkt Samia kwenye halmashauri ya wilaya Mbeya mwaka huu ‘sequip’. Halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi milioni 583 kwa ajili ya ujenzi wa shule hii, ambayo itachukua wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne.
Shule ya Lwanjilo itakuwa na madarasa nane (8) ambayo yanauwezo wa kubeba wanafunzi 50 katika kila darasa na kuleta jumla ya wanafunzi 400 watakaosoma shuleni hapo, shule itakuwa na maabala tatu za kisasa, maabala ya fizikia,biolojia na kemia ambazo wanafunzi wa sayansi watapata mafunzo ya vitendo.
Pia shule itakuwa na ofisi ya mwalimu mkuu na walimu wa taaluma, vyoo vya walimu na wanafunzi ambavyo vya wanafunzi vitakuwa kumi na moja (11), vya wanafunzi wa wakiume matundu 5 na wakike matundu 6.
Mchakato wa kusajili shule hii tayari umeanza na tarehe 30 Octobaujenzi wa shule hii utakuwa umekamilika na kuanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka ujao wa masomo 2024.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.