Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amebainisha mikakati ya kutokomeza ajali mkoani Mbeya akiwa kwenye ziara ya kikazi Julai 25, 2018.
Mhe. Samia amesema mikakati hiyo ni ya muda mrefu na muda ambapo Serikali itatengeneza barabara ya magari makubwa na magari madogo.
Makamu wa Rais ameitaja mikakati hiyo alipokuwa anatoa pole kwa wananchi katika eneo la Mbalizi lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kuwa mpango wa muda mfupi ni kutengeneza barabara ya magari madogo ya St. Marcus-Mbalizi.
“Tumeamua magari makubwa yapite barabara yake na magari madogo yapite kwenye barabara yake kwa kuyatengenezea njia zao maalumu. Lakini hili la kutengeneza barabara ya magari makubwa ni utekelezaji wa muda mrefu, hivyo kwa muda huu tunatengeneza barabara ya magari madogo, ikikamilika magari madogo yote yatapita katika barabara hiyo na barabara hii inayotumika sasa yatabaki magari makubwa tu mpaka barabara yao itakapokamilika”
Ajali katika mkoa wa Mbeya zimekuwa zikitokea mara kwa mara kwa kuhusisha magari makubwa na madogo, ambapo kwa mwezi Juni 2018 jumla ya ajali tatu zimetokea na kusababisha vifo vya watu 45.
Aidha Makamu wa Rais, amesema atafanya ziara ya kutembelea mkoa wa Mbeya kwa muda wa siku sita kuanzia Julai 25 hadi Julai 30 ambapo atatembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya zote.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.