“Mbeya bila udumavu inawezekana” Hii ni kauli mbiu ya kuhamasisha mwezi wa lishe katika mkoa wa Mbeya ambao unaadhimishwa mara mbili kwa mwaka; Juni na Disemba.
Akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya, Ndg. Ferister Zanzibar kwenye uzinduzi wa lishe mwezi june amesema kuwa, tatizo la udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano (5) katika mkoa wa Mbeya ni kubwa sana ukilinganisha na mikoa mingine. Takwimu za 2015-2016 zinaonesha udumavu katika mkoa wa Mbeya ni asilimia 37.7 ukilinganisha na asilimia 34.4 ya taifa kwa ujumla.
Aidha Zanzibar amesema kwamba licha ya mkoa wa Mbeya kuongoza uzalishaji wa mazao ya chakula pamoja na mbogamboga lakini bado tatizo hili linaendelea kuwa sugu kutokana na tamaduni za wanaume wengi katika familia kuwaachia wanawake pekee jukumu la kuwahudumia watoto.
“Wananchi, hususani kina baba ni jukumu letu sote kuhakikisha tunawapa watoto wetu virutubisho muhimu na sio kuwaachia kina mama peke yao. Inatakiwa baba ashirikiane na mama kwa namna moja ama nyingine kuhakikisha kwamba mtoto anapata vipimo sahihi”
Awali akisoma risala Kaimu Afisa Lishe, Julith Shirima amesema kuwa, katika mwezi huu halmashauri itatoa huduma za lishe bure kwa watoto chini ya miaka 5. Amezitaja huduma zitakazotolewa kuwa ni pamaja na; kupima hali ya lishe, kutoa matone ya vitamin A na dawa za kutibu minyoo, huduma ya unasihi na kutoa elimu ya usafi wa chakula, maji na mazingira.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.