Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya mbeya imepitisha kiasi cha shilingi bilioni 43 katika makusanyo na matumizi kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Katika bajeti hii inapendekeza kuwepo kwa baadhi ya miradi ya kipaumbele ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kituo cha afya cha wilaya, kufanya ukarabati wa wa stendi pamoja na ununuzi wa lori litakalo tumika kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali.
Shughuli zitakazo tekelezwa katika mwaka huo ni pamoja na kuendelea kutoa mikopo ya wanawake, vijana na walemavu, ukarabati wa miundombinu ya halmashauri, kuendeleza ujenzi wa hospitali ya wilaya pamoja na kufidia maeneo kwaajili ya matumizi mbalimbali ya Halmashauri.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.