Baraza la Madiwani katika halmashauri ya wilaya ya mbeya limefanya kikao cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/2023 huku agenda kuu za baraza hilo ni kujadili taarifa ya utendaji na uwajibikaji wa halmashauri kwa mwaka 2022/2023 uchaguzi wa makamu mwenyekiti, muundo wa kamati za kudumu za halmashauri kwa mwaka 2023/2024 na kupitisha ratiba ya vikao vya halmashauri kwa mwaka 2023/2024.
Kwa upande wa mapato, halmashauri imefanikiwa kukusanya jumla ya Shilingi. 5,150,921,688.57 sawa na asilimia 107 ya lengo ambalo lilikuwa ni Shilingi. 4,810,300,000.00hivyo kutokana na kukusanya fedha hizo, halmashauri imeweza kuchangia jumla ya Shilingi. 1,603,317,661.00 sawa na asilimia 104 ya Shilinhi.1,588,400,000.00 iliopangwa kwenda kwennye miradi mbalimbali ya maendeleo iknayotekelezwa katika taasisi mbalimbali ngazi ya kata na vijiji.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.