Baraza la madiwani Halmashauri ya wilaya ya Mbeya imepitisha mapendekezo ya sheria ndogo zitakazo kuwa zinasimamia mambo ya usafi wa mazingira, ukusanyaji wa mapato, pamoja na utoaji wa huduma za kiafya.
Zoezi hilo la kupitisha sheria ndogo katika ngazi ya baraza la madiwani limefanyika agosti 22, 2018 katika ukumbi wa halmasauri kwenye baraza la madiwani la robo ya nne.
Akitoa taarifa ya baadhi ya sheria ndogo zilizopendekezwa Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Ndg. Wilson Nyamunda amesema kuwa sheria hizo zitaiongezea halmashauri uwezo na ufanisi katika kusimamia shughuli zake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Mhe. Mwalingo Kisemba amesema kuwa halmashauri imeshatekeleza wajibu wake, kinachosubiriwa kwa sasa ni mapendekezo hayo kupelekwa ngazi za juu kwa ajili ya mapitio na kupitishwa kabla haijaanza kutumika.
Kwa mujibu wa kanuni na utaratibu wa utungaji wa sheria ndogo katika mamlaka ya Serikali za mitaa, sheria ikipitishwa na baraza la madiwani inapelekwa ofisi ya mkoa kwa ajili ya kupata maoni. Kisha ngazi inayofuata inapelekwa kwa waziri mwenyedhamana kwa ajili ya kuthibitisha na baadae kwenda kwa mwanasheria mkuu wa Serikali kuona kama haipingani na sheria nyingine, kisha inapelekwa kwa mhariri wa serikali kwaajili ya kuhariri maneno na mwisho inatangazwa kwenye gazeti la serikali tayari kwa matumizi.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.