Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Mbeya limepitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 huku ikitegemea kukusanya kiasi cha shilingi 4.3 bilioni kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani.
Akiwasilisha rasimu ya bajeti ya mwaka 2022/2023 mbele ya baraza la madiwani Afisa Mipango wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Ndg. Filbert Mbwilo amebainisha kuwa kwa halmashauri ya wilaya ya Mbeya inatarajia kukusanya na kutumia jumla ya shilingi 64,671,904,837.07 kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani serikali kuu na wahisani.
Katika rasimu ya bajeti bajet hii imependekezwa kuwa na mradi mmoja wa maendeleo.Katika kutekeleza adhma hii kiasi ya shilingi 500,000,000.00 kimetengwa kwajili ya ujenzi wa kituo cha Afya kitakacho jengwa eneo la Mamlaka ya mji mdogo Mbalizi. Aidha mradi huu utakua kipaumbele cha halmashauri ya wilaya ya mbeya katika mwaka wa fedha 2022/2023
Baadhi ya madiwani wameona kuwa bajeti hiyo inatoa matumaini kuwa huenda ikawavusha kwani imejaribu kugusa katika kila maeneo kama ya Elimu, Afya na kilimo.
“Bajeti hii imegusa kila maeneo ya wananchi tunaona mwelekeo kujenga kituo cha Afya Mamlaka ya mji mdogo mbalizi ambacho kitakua msaada mkubwa sana kwa wananchi wa eneohilo na kata jirani pia kitachangia ongezeko la mapato ya ndani ya halmashauri ” Mhe. Eng. Boniface S. Njombe Diwani kata ya Ulenje
“Nimefurahishwa sana na hii bajeti kwani inaonesha mwelekeo wa kupambana na ukatili wa kijinsia katika eneo letu, pia imezingatia sana changamoto za wanafunzi wakike katika shule zetu ” Mhe. Pili A. Mwatowe Diwani viti maalum.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.