Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Mbeya limepitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022 huku ikitegemea kukusanya kiasi cha shilingi 3.9 bilioni kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani.
Katika bajeti ya mwaka huo, mapendekezo ya matumizi ya fedha husika yakiwa kwenye miradi ya kimkakati itakayoiingizia halmashauri mapato ambayo ni ujenzi wa shule ya mchepuo wa kingereza na uwezeshaji kilimo cha parachichi.
Akiwasilisha taarifa hiyo ya rasmu ya bajeti kwa mwaka husika mbele ya baraza la madiwani naye Afisa Mipango wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Ndg. Filbert Mbwilo amebainisha kuwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 halmashauri ya wilaya ya Mbeya inatarajia kukusanya na kutumia jumla ya shilingi 56,498,189.15 kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani , serikali kuu na wahisani.
Baadhi ya madiwani wameona kuwa bajeti hiyo inatoa matumaini kuwa huenda ikawavusha kwani imejaribu kugusa katika kila maeneo kama ya Elimu, Afya na kilimo.
“Bajeti hii imegusa kila maeneo ya wananchi tunaona mwelekeo kujenga shule ya halmashauri tunategemea kuwa na halmashauri ambayo inaenda kujitegemea” Ibrahimu Mwakasege, diwani wa kata ya Ilungu.
“Nimefurahishwa sana na hii bajeti kwani inaonesha mwelekeo wa kupambana na ukatili wa kijinsia katika eneo letu” mwananchi wa kata ya Inyala Felister Kaisi.
Mbaliz Road
Sanduku la posta: 599
Simu ya mezani: 025-2502260
Simu ya mkononi: 0762210758
Baruapepe: ded@mbeyadc.go.tz/info@mbeyadc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya District Coucil . All rights reserved.